Thursday, June 28, 2018

ASASI YA WATU NA WANYAMA (TPW), YAIWEZESHA BAWAKIMO SH MILIONI 40 ZA MRADI WA UHIFADHI MAZINGIRA NA UFUGAJI WA NYUKI

Msimamizi wa miradi wa Asasi ya Watu na Wanyama ya (TPW), iliyopo Simanjiro mkoani Manyara akizungumza wakati wa kukabidhi mradi mpya wa uhifadhi mazingira na ufugaji nyuki kwa Baraza la Wanawake wa Kikufugaji Monduli (BAWAKIMO), Asasi hiyo imewapa Sh milioni 40 kama mtaji kwa  wanawake 250 wa Kata ya Lemooti na Mswakini  wilayani Monduli.

Monday, June 4, 2018

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI (TAWA), YAMWANGA MILIONI 50 UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI YA UFUNDI SIMIYU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akielezea kwa wanahabari faida na umuhimu wa Pori la Akiba la Maswa, lililowezesha kupitia mapato yanayokusanywa kupitia shughuli za utalii wa picha na uwindaji wa kitalii kuchangia mkoa huo Sh milioni 50 za ujenzi wa majengo ya Shule ya  maalumu ya vipaji ya Sekondari ya Ufundi Simiyu inayojengwa mjini Bariadi.Fedha hizo zilitolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA)

Friday, May 18, 2018

MBIO ZA MARATHONI MUSKATHLON INTERNATIONAL NA COMPASSION INTERNATIONAL TANZANIA ZAFANYIKA MKOANI KILIMANJARO

Baadhi ya washiriki wa mbio za marathoni kutoka Ujerumani na Uswis Muskathlon International ikishirikiana na Shirika la Compassion Tanzania wafanikiwa kuhitimisha mbio hizo zilizolenga kuchangia fedha kwa ajili ya watoto wahitaji nchini Tanzania wanaolelewa katika vituo vya Shirika la Compassion. Mbio hizo za kukimbia, kuendesha baiskeli na kutembea zilizofanyika Kijiji cha Roo, Hai mkoani Kilimanjaro

Wednesday, May 16, 2018

TANZANITE ONE YAKUBALI KUILIPA SERIKALI FIDIA, KODI WATAKAYOKUBALIANA



Ikulu, Dar es Salaam.

Kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzanite One imekubali kuilipa Serikali fidia pamoja na kodi watakayokubaliana kutokana na dosari zilizokuwepo hapo awali.

Saturday, May 5, 2018

KIKAO KAZI CHA WAKUU WA HIFADHI ZA TAIFA NCHINI CHAFANYIKA MOROGORO

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini Marijani Nsato amefungua kikao kazi cha Wakuu wa Hifadhi za Taifa nchini pamoja na Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa yote inayopakana na Hifadhi za Taifa na kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano ili kumaliza changamoto ya ujangili kwenye hifadhi.

Monday, April 30, 2018

TANAPA YACHANGIA MILIONI 50 UJENZI SEKONDARI YA UFUNDI SIMIYU



Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh milioni 50, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka, kushoto ni Meneja Uhusiano wa TANAPA Paschal Shelutete na kulia mwisho ni Mkuu wa wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga. 

Monday, April 23, 2018

COMMERCIAL BANK OF AFRICA (CBA) TANZANIA, IPO IMARA NA SALAMA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 100

Afisa Mtendaji Mkuu wa Commercial Bank of Africa (CBA) Tanzania, Gift Shoko akizungumza na wateja wa benki hiyo mkoani Arusha wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa lengo la kuwashukuru kwa kuendelea kuwaamini, kuwaelezea maendeleo yanayotokea na kupokea mrejesho kutoka kwa wateja wao, halfa hiyo ilifanyika Mount Meru Hoteli mjini hapa. 

Sunday, April 15, 2018

MAONYESHO YA SEKTA YA UTALII YAJULIKANAYO KARIBU KILIFAIR KUFANYIKA JUNI 1 HADI 3, MWAKA HUU MJINI MOSHI

Wakurugenzi Watendaji wa KILIFAIR wa kwanza kulia Dominic Shoo na watano kutoka kulia Tom Kunkler, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wao wakati wa hafla ya kutambulisha maonyesho ya utalii yajulikanayo kama KARIBU KILIFAIR yatakayofanyika mjini Moshi Juni 1 mpaka 3, mwaka huu. Hatua hiyo imekuja baada ya kuungana kwa KARIBU FAIR na KILIFAIR.

Tuesday, April 10, 2018

JENGO la kitega uchumi la Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro jijini Arusha ambalo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka huu litakuwa kivutio cha kihistoria cha utoaji wa huduma za utalii hapa nchini.


Na Hamza Temba - WMU
........................................................
JENGO la kitega uchumi la Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro jijini Arusha ambalo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka huu litakuwa kivutio cha kihistoria cha utoaji wa huduma za utalii hapa nchini.

NDEGE VIVUTIO VINAVYOCHANGIA KUIMARISHA MAPATO KWENYE SEKTA YA UTALII NCHINI



JAMII nchini imetakiwa kuwatunza na kuwalinda ndege waliopo kutokana na kuwa sehemu ya vivutio vinavyochangia kuimarisha mapato kwenye sekta ya utalii.

ASASI YA NATURE TANZANIA YAHAMASISHA KUTUNZA NDEGE KWA AJILI YA UTALII


Baadhi ya wafanyakazi, watafiti wa masuala ya uhifadhi na utalii na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Nature Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mjini Arusha 

Monday, April 9, 2018

RC GAMBO AAGIZA KILA HALMASHAURI ARUSHA IPANDE MITI MILIONI 1.5 KWA MWAKA



Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameziagiza halmashauri zote za mkoani humo  kupanda miti milioni 1.5 kwa mwaka ili kutunza mazingira.

Sunday, April 8, 2018

HOTELI ZA CHEMCHEM ZAWAPIGA MSASA WAFANYAKAZI WAKE



Mwalimu John Macha

VYUO vinavyotoa elimu ya utalii nchini vimetakiwa kuboresha mitaala ili kuzalisha wafanyakazi watakaokuwa na uhitaji na ushindani wa kupambana na mataifa mengine katika sekta ya utalii.

Thursday, March 29, 2018

MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI (MOCU) PROF ,FAUSTINE BEE AZINDUA NA KUONGOZA WATUMISHI WENZAKE WA CHUO HICHO KATIKA ZOEZI LA UPIMAJI WA HOMA YA INI.


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Mosi (MoCU) Prof ,Faustine Bee akizungumza wakati wa uzinduzi wa Upimaji wa Homa ya Ini kwa Watumishi wa Chuo hicho pamoja na Wategemezi wao, zoezi ambalo linafanyika katika kituo cha Afya kilichopo chuoni hapo . 

AGPAHI YAKABIDHI MASHINE ZA KUCHUNGUZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI,KOMPYUTA MKOA WA MWANZA



Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) limekabidhi mashine tano za kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ‘cryotherapy machines’ mkoa wa Mwanza.

KLABU ZA BIASHARA MWAROBAINI WA TATIZO LA AJIRA TANZANIA YA VIWANDA


 Mkurugenzi wa Shule ya Ester Memorial Academy

-ARUSHA
ELIMU ya ujasiriamali kupitia Klabu za Biashara inayolenga wanafunzi wa Shule za Msingi,Sekondari na Vyuo kujifunza kwa vitendo, kuweka akiba na kupata kipato imetajwa kuwa ni mwarobaini wa tatizo la ajira nchini.

Wednesday, March 21, 2018

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, MHE. JAPHET HASUNGA AZINDUA MABASI MAWILI MAPYA YA WIZARA HIYO MJINI DODOMA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Japhet Hasunga akiendesha moja ya basi hilo kama ishara ya uzinduzi.

ATUMIA MIEZI SABA KUSAFIRI KWA PIKIPIKI KUTOKA OMAN HADI TANZANIA, ATEMBELEA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII MJINI DODOMA

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akiteta jambo na Maher Al Barwani kutoka nchi ya Oman mwenye asili ya Tanzania ambaye amesafiri kwa muda wa miezi saba kupitia mataifa mbalimbali hadi kufika Tanzania kwa pikipiki kwa lengo la kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania nchini humo, alipotembelea ofisi za Wizara hiyo mjini Dodoma.