Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu Genesta Mhagama akiwa na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo wakati
wa uzinduzi wa namba maalum ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti ukimwi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Genesta Mhagama amemkabidhi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selamani Jaffo
Sh milioni 200,000 kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha Afya Mererani ikiwa ni ahadi
ya Rais Dk. John Magufuli aliyoitoa wakati waziara yake mkoani humo mwezi uliopita.