Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akizungumza na wanahabari hawapo pichani kuhusu maendeleo yaliyofanywa mkoani kwake kutokana na fedha zinazotokana na shughuli za utalii wa picha na uwindaji wa kitalii katika Pori la Akiba la Maswa
Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA), Twaha Twaibu akizungumza na wanafunzi wa Sekondari ya Simiyu mara baada ya msafara wa Ofisa elimu na maofisa wa Wanyamapori mkoani humo kutembelea shughuli za ufyatuaji matofali zinazoendelea kufanywa shuleni hapo tayari kwa ujenzi wa sekondari ya Ufundi ya Simiyu
Baadhi ya wanafunzi wa Sekonari ya Simiyu wakiwasilikiza maofisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA), wakati wa ziara ya kutembelea maandalizi ya ujenzi wa sekondari ya vipaji maalumu ambapo Mamlaka hiyo ilichangia Sh milioni 50 kwa ajili ya ufyatuaji wa matofali
Mkuu wa Sekondari ya Simiyu Mwalimu Paul Susu akiwaonyesha baadhi ya tofali zinazoendelea kufyatuliwa shuleni hapo ili kuanza ujenzi wa majengo mengine mapya
Baadhi ya vijana waishio katika Mji wa Bariadi mkoani Simiyu wakiendelea na ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya ujenzi wa Sekondari ya vipaji maalumu ya Simiyu
Majengo ya Shule ya Sekondari Simiyu inayoendelea kujengwa kwa msaada wa wadau mbalimbali wa maendeleo wakiwamo Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini TAWA iliyochangia kiasi cha Sh milioni 50
Mkuu wa Sekondari ya Simiyu Mwalimu Paul Susu akiwaonyesha baadhi ya misingi iliyochimbwa na wananchi wa mjini Bariadi kwa kujitoleaa shule hiyo inajengwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ikiwamo nguvu za wananchi
Muonekano wa Sekondari ya Simiyu pichani
No comments:
Post a Comment