Friday, May 18, 2018

MBIO ZA MARATHONI MUSKATHLON INTERNATIONAL NA COMPASSION INTERNATIONAL TANZANIA ZAFANYIKA MKOANI KILIMANJARO

Baadhi ya washiriki wa mbio za marathoni kutoka Ujerumani na Uswis Muskathlon International ikishirikiana na Shirika la Compassion Tanzania wafanikiwa kuhitimisha mbio hizo zilizolenga kuchangia fedha kwa ajili ya watoto wahitaji nchini Tanzania wanaolelewa katika vituo vya Shirika la Compassion. Mbio hizo za kukimbia, kuendesha baiskeli na kutembea zilizofanyika Kijiji cha Roo, Hai mkoani Kilimanjaro

Mshiriki wa mbio za kuchangia watoto wenye uhitaji akionyesha Medali yake baada ya kufanikiwa kumaliza 
 Washiriki wa mbio za Muskathlon wakifurahia na Medali zao baada ya kumaliza kukimbia  


 Mshiriki akimalizia mbio katika Kijiji cha Roo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro 



 Washiriki wakifurahia kumaliza mbio za maradhoni zilizofanyika mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kuchangia fedha kwa ajili ya watoto wahitaji wanaofadhiliwa na Shirika la Compassion Tanzania
 Mwendesha baiskeli akiendelea kukata upepo Kilometa 120 lengo likiwa ni kuchangia fedha kwa ajili ya watoto wahitaji chini ya Shirika la Compassion Tanzania

Washiriki wa kutembea kwa miguu Kilometa 63 wakiendelea na kutekeleza wajibu huo ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwa ajili ya watoto wahitaji Tanzania wanaolelewa na Shirika la Compassion Tanzania
 Mwanariadha Josephat Joshua akifurahia kumaliza mbio za Nusu Marathoni Kilometa 21 zilizolenga kuchangia watoto wahitaji wanaolelewa na Shirika la Compassion Tanzania 
 Mwanariadha Josephat Joshua akipewa maelezo mara baada ya kumaliza mbio za nusu marathoni 
 Hawa ni matunda ya Shirika la Compassion Tanzania kwa pamoja walishiriki katika kukimbia mbio za Nusu Marathoni Kilometa 21 huko Roo, Hai mkoani Kilimanjaro


Mkurugenzi wa Shirika la Compassion Tanzania Agnes Hotay akielezea malengo ya kufanyika kwa mbio hizo na namna fedha zitakazopatiokana zitakavyotumika kuwasaidia watoto wote waliopo kwenye vituo vilivyo chini ya Makanisa ya Kiinjili nchini.
Kiongozi wa Shirika la Muskathlon kutoka Ujerumani Ralf Pieper akielezea malengo na madhumuni ya kuandaa mbio hizo ambapo shirika hilo kupitia wanachama wake wamekuwa wakifanya kazi ngumu kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia watoto wenye mahitaji na masuala mengine
Mwanariadha Josephat Joshua akihojiwa na vyombo vya habari kuhusu ushiriki wake kwenye mashindani hayo ambapo alikuwa mshindi wa kwanza mbio za Kilometa 21 

No comments:

Post a Comment