Saturday, May 5, 2018

KIKAO KAZI CHA WAKUU WA HIFADHI ZA TAIFA NCHINI CHAFANYIKA MOROGORO

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini Marijani Nsato amefungua kikao kazi cha Wakuu wa Hifadhi za Taifa nchini pamoja na Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa yote inayopakana na Hifadhi za Taifa na kuwataka kufanya kazi kwa ushirikiano ili kumaliza changamoto ya ujangili kwenye hifadhi.


Kamishna Nsato ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa ametoa wito huo leo mjini Morogoro na kuagiza kuwa ushirikiano ni jambo la kipaumbele cha kwanza  kwa kuwa wote ni walinzi muhimu katika kulinda rasilimali zinazopatikana katika maeneo yaliyotengwa kisheria kama Hifadhi za Taifa.

Kamishna Nsato:
#Katika mwaka wa fedha2016/2017 jumla ya majangili 4,294 walikamatwa.
# Idadi ya silaha zilizokamatwa ni pamoja na SMG 9, Riffles 19, Magobore 55, Shortgun 18, waya za kutega wanyama 84,817.
# Tembo waliouawa ni 15 pamoja na ukamatwaji wa mifugo 77,817.
# TANAPA itaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya dola katika kukabiliana na changamoto ya ujangili nchini.
# TANAPA itaendelea kushirikiana na jamii kupitia Mpango wa Ujirani Mwema ili kuwawezesha wananchi kushiriki kulinda wanyamapori nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi:
# Jukumu la kulinda rasilimali zilizopo hifadhini ni la wananchi wote.
# TANAPA itaendeleza ushirikiano mzuti baina yake na Jeshi la Polisi nchini.
# Kikao hiki kinalenga kujenga uelewa wa pamoja wa kulinda Hifadhi za Taifa na rasilimali zinazopatikana hifadhini.
# Silaha haramu ni kichocheo kikubwa cha ujangili nchini.

 TANAPA itaendelea kusimamia sheria zinazosimamia hifadhi ili rasilimali za wanyamapori na mimea ziendelee kuwa na tija kwa uchumi wa nchi yetu.

No comments:

Post a Comment