Wednesday, May 9, 2018

COMPASSION INTERNATIONAL TANZANIA (CIT) NA INTERNATIONAL MUSKATHLON WAANDAA MBIO ZA MARATHONI KWA LENGO LA KUCHANGISHA FEDHA KWA WATOTO MASIKINI NCHINI. MASHINADANO HAYO YANATARAJIWA KUFANYIKA MEI 17, MWAKA HUU ENEO LA ROO MKOANI KILIMANJARO

 
 Washiriki wa mbio za kuchangisha ili kupata fedha kwa ajili ya watoto masikini 

 Washiriki wakiendelea kuchukuana 
 Washiriki wa mbio za Baiskeli 


Zaidi ya wageni 70 kutoka nchi ya Ujerumani na Uswisi pamoja na  Watanzania 70 wanatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo yanayolenga kutafuta wafadhili kwa ajili ya watoto wahitaji wa Nchini Tanzania.

Nchi nyingine Sita zilizopo kwenye mpango huo barani Afrika Kenya,Uganda,Rwanda, Ethiopia,Bukinafaso na Ghana.

Mashindano hayo yatahusisha Mbio za  Marathoni  Kilometer 21(half marathoni) na Kilometer 42(full marathoni), Kutembea Kilometer 63 na waendesha baiskeli Kilometer 120.

Kila mgeni anatakayeshiriki  atatakiwa kuchangia kiasi cha Euro 10,000 au kuwatafutia wafadhili watoto 10.

Fedha itakayopatikana itaelekezwa Shirika la Compassion International Tanzania kwa ajili ya kukidhi mahitaji mbalimbali ya watoto kupitia Makanisa ya Kiinjili Tanzania yaliyo katika ushirika wenza na Compassion International Tanzania.




No comments:

Post a Comment