Wednesday, March 21, 2018

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, MHE. JAPHET HASUNGA AZINDUA MABASI MAWILI MAPYA YA WIZARA HIYO MJINI DODOMA

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Japhet Hasunga akiendesha moja ya basi hilo kama ishara ya uzinduzi.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Japhet Hasunga amezindua rasmi mabasi mawili aina ya TATA kwa ajili kutoa huduma za usafiri wa kwenda na kurudi kazini kwa Watumishi wa Wizara hiyo walioko mjini Dodoma.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Naibu Waziri Hasunga amesema mabasi hayo yatasadia kukabiliana na changamoto ya usafiri iliyokuwepo hususan kwa wale watumishi wa Wizara wanaotumia ofisi zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Aidha, ametoa wito kwa madereva na watumishi watakaotumia mabasi hayo kuyatunza ili yaweze kudumu kwa muda mrefu.
Mabasi hayo ya uwezo wa kuchukua abiria 91 wakiwa wamekaa ambapo basi moja kubwa lina uwezo wa kuchukua abiria 51 na lingine dogo abiria 40.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Tutubi Mangazeni amesema mabasi hayo yatatumika pia kwa ajili ya shughuli nyingine za Kiserikali ikiwemo kuwasafirisha Watumishi wa Umma watakaohitaji kutembelea maeneo ya Hifadhi na kushirikia kwenye michezo mbalimbali hapa nchini.
Mabasi hayo yamegharimu jumla ya Shilingi Milioni 232 za Kitanzania.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Japhet Hasunga (kulia), Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Utawala, Tutubi Mangazeni wakiwa wameketi kwenye viti vya moja ya basi hilo baada ya uzinduzi.
 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (nyuma) akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Aloyce Nzuki kukagua moja ya basi hilo.

No comments:

Post a Comment