Thursday, June 28, 2018

ASASI YA WATU NA WANYAMA (TPW), YAIWEZESHA BAWAKIMO SH MILIONI 40 ZA MRADI WA UHIFADHI MAZINGIRA NA UFUGAJI WA NYUKI

Msimamizi wa miradi wa Asasi ya Watu na Wanyama ya (TPW), iliyopo Simanjiro mkoani Manyara akizungumza wakati wa kukabidhi mradi mpya wa uhifadhi mazingira na ufugaji nyuki kwa Baraza la Wanawake wa Kikufugaji Monduli (BAWAKIMO), Asasi hiyo imewapa Sh milioni 40 kama mtaji kwa  wanawake 250 wa Kata ya Lemooti na Mswakini  wilayani Monduli.

Mkurugenzi wa Baraza la Wanawake wa Kifugaji Monduli (BAWAKIMO), Mary Morindat akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa uhifadhi mazingira na ufugaji nyuki kwa wanawake wa 250 kutoka Kata ya Lemooti na Mswakini wilayani humo
Msimamizi wa miradi wa Asasi ya Watu na Wanyama ya (TPW), iliyopo Simanjiro mkoani Manyara akizungumza wakati wa kukabidhi mradi mpya wa uhifadhi mazingira na ufugaji nyuki kwa Baraza la Wanawake wa Kikufugaji Monduli (BAWAKIMO), Asasi hiyo imewapa Sh milioni 40 kama mtaji.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimanta akizungumza wakati wa ufunguzi wa mradi wa uhifadhi mazingira na ufugaji wa nyuki wilayani humo.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimanta akipokea mfano wa Hundi ya zaidi ya Sh milioni 40 kutoka kwa Msimamizi wa Miradi wa Asasi ya Watu na Wanyama (TPW),Revocatus Magayane kwa ajili ya mtaji wa mradi wa ufugaji nyuki kwa wanawake 250.
Mkuu wa wilaya ya Monduli Iddi Kimanta akibadilishana mawazo na Msimamizi wa Miradi wa TPW Revocatus Magayane mara baada ya kukabidhi mradi wa ufugaji nyuki kwa wanawake 250 wa Kata ya Lemooti na Mswakini. 
Mratibu wa Miradi kutoka BAWAKIMO Angela Kagashe akizungumza na baadhi ya wanawake wanachama wa baraza hilo juu ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo mpya wa uhifadhi mazingira na ufugaji wa nyuki wilayani Monduli. 

No comments:

Post a Comment