-ARUSHA
ELIMU ya ujasiriamali kupitia Klabu za Biashara inayolenga wanafunzi wa Shule za Msingi,Sekondari na Vyuo kujifunza kwa vitendo, kuweka akiba na kupata kipato imetajwa kuwa ni mwarobaini wa tatizo la ajira nchini.
Hayo yalisemwa mjini hapa juzi na Mkurugenzi wa Shule ya Ester Memorial Academy iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha Wilfred Hume alipokuwa akifunga mafunzo ya Klabu za biashara kwa wanafunzi 685 wa shule 20 zilizopo Arusha.
Akizungumza na wanafunzi, walezi wa klabu na walimu Hume alisema, wazo hilo linalenga kuwajengea uwezo wa wanafunzi kujitegemea linapaswa kusambazwa nchi nzima badala ya maeneo machache.
“Programu hii ina faida tumeiona ikibadilisha mitazamo ya watoto shuleni inaweza kuwa mtatuzi wa tatizo la soko la ajira kwa wanafunzi wanaomaliza masomo na kukaa wakisubiria ajira,” alisema Mwalimu Hume na kuongeza:Mwalimu Mlezi Klabu ya Biashara
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki
“Elimu hii ya ujasiriamali isisubiri mtu akishakuwa mkubwa au akimaliza masomo yake ndipo aanze kufundishwa badala yake iwekezwe sasa kwenye vichwa vya wanafunzi wakiwa bado wadogo,” alisema.
Mwalimu Hume ambaye ni mlezi wa Klabu ya biashara shuleni hapo alisema, mpango huo endapo wanafunzi mashuleni watauelewa utakuwa faida kubwa kwa wazazi.
“Wanafunzi waliopata mafunzo kupitia klabu za biashara shuleni baada ya vipindi vya masomo ya darasani huingia kwenye ujasiriamali kwa vitendo na kupitia mawazo waliyobuni huweza kutengeza bidhaa ambazo baadaye huziuza na kuingiza kipato chao,”
“Elimu hii haitachanganyana na masomo mengine, mpangilio na utaratibu uliofanyika mashule za majaribio 20 haujawahi kuleta mgongano tangu ulipoanzishwa mwaka 2017,” alisema Mwalimu Hume.
Kwa
upande wake mshauri wa elimu fedha Shirika la Opportunity International George
Kipangula alisema, mradi huo ulianza mwaka 2012 Morogoro na Iringa ambapo kwa
sasa unatekelezwa mkoani Arusha.
“Nadharia
ya Klabu za Biashara ni kujifunza kwa vitendo, kuweka akiba na pamoja na kupata
kipato. Mwanafunzi akipita kwenye mpango huu anakuwa tofauti kabisa na mwingine
“Mwanafunzi
ambaye hajapita klabu za biashara anabaki na elimu ya vyeti na si vitendo.
Mwanafunzi huyo akimaliza masomo anaweza asiuzike katika soko la ajira au soko
la kujitegemea.
George Kipangula
“Anapopitia
elimu hii mwanafunzi anatimiza Falsafa ya Baba wa Taifa, Mwal. Julius Nyerere ya
Ujamaa na Kujitegemea. Leo hii kuna wanafunzi wanaomaliza masomo wakiwa bado ni
tegemezi,” alisema Kipangula.
Alisema
programu hiyo iliyoanza Septemba 2017 hadi Machi 2018 ilifanywa Shirika la
Opportunity International kwa kushirikiana na Fundacion Paraguaya wafadhili wa
mradi huo.
Alisema
tangu kuanza kwa programmu hiyo klabu za biashara zimewezesha wanafunzi kupata
mbinu za uongozi na biashara wakiwa bado mashuleni hatua ambayo awali hawakuwa
nayo.
“Wanafunzi
waliopita klabu za biashara wamekuwa na ubunifu wa hali ya juu wanatafuta
ufumbuzi wao ndani ya muda mfupi katika kutengeneza mawazo ya biashara,” alisema
Kipangula.
Naye
Mkuu wa Shule ya Nalopa iliyopo Njiro mjini Arusha Milsent Samali alisema,
changamoto wanayoipata kwa sasa ni watoto kushindwa kufanya kazi za mikono
wakiwa mashuleni.
Mkuu wa Shule ya Nalopa akizungumza
“Hatuwezi
kusema watoto ndio waliosababisha athari hii bali ni wazazi waliopo majumbani.
Watoto wengi hawajui kushika majembe wala kufanya usafi shuleni.”
“Kama
tunataka kweli kwenda kwenye uchumi wa viwanda na uchumi wa kati ni lazima
tubadilishe mfumo wa elimu. Tutoke kwenye habari ya karatasi na kwenda kwenye
vitendo zaidi ili watoto wajifunze wakiwa shule ya msingi,” alisema Mwalimu
Samali.
Mwisho
No comments:
Post a Comment