Mwalimu John Macha
VYUO vinavyotoa elimu ya utalii nchini vimetakiwa kuboresha
mitaala ili kuzalisha wafanyakazi watakaokuwa na uhitaji na ushindani wa kupambana
na mataifa mengine katika sekta ya utalii.
Aidha imebainika kwamba kuwapo kwa uhaba wa wafanyakazi wenye
sifa mahiri katika sekta hiyo kumechangia kama taifa kushindwa kupambana na
nchi nyingine katika kuvutia watalii.
Akizungumza kwenye mafunzo hayo Meneja wa Chemchem Foundation,
Charles Sylvesta alisema , wameamua kuendesha mafunzo kwa wafanyakazi wao zaidi
ya 160 ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo ili waweze kukabiliana na changamoto
mbalimbali.
"Mafunzo haya yamejumuisha kuwapiga msasa kwenye lugha ya
Kiingereza, upishi, kuandaa vyumba vya kulala watalii na kuongoza watalii kupitia
wataalam wa ndani na nje ya nchi,"alisema Sylvesta.
Kwa upande wake Mwalimu aliyekuwa akitoa mafunzo hayo Aidha
kwenye mafunzo hayo,Mwalimu wa Lugha kwenye hoteli hizo, John Macha
alisema, baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu
kuwasiliana na watalii.
"Mafunzo haya tumeyaendesha kwa sasa kutokana na mazingira
kuturuhusu kwani hatuna wageni wengi, hivyo tumeamua kutumia fursa hii
kuendesha mafunzo haya ikiwa lugha mbalimbali za kimataifa.
“Mafunzo haya yatasaidia wao kuwasiliana vizuri zaidi na watalii
au wageni wetu wanaotembelea vivutio na kulala hotelini kwetu, "alisema
Naye Katibu Mtendaji wa Chama cha waajiri katika nchi za Afrika
ya Mashariki(EAEO) Dk Aggrey Mlimuka, akielezea kuhusu tatizo la uhaba wa
wafanyakazi wa sifa linazozikabili nchi za Afrika ya Mashariki alisema,
takribani nusu wa wahitimu wa Vyuo vikuu hawana sifa stahiki
katika soko la ajira.
Wakati huo huo Meneja wa Chemchem Lodge Kelly Ricklan
alisema mafunzo hayo, yatawasaidia wafanyakazi hao wanaoishi katika eneo la
Burunge kupata uwezo wa kufanyakazi kitaalamu zaidi badala ya mazoea.
No comments:
Post a Comment