Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameziagiza halmashauri zote za
mkoani humo kupanda miti milioni 1.5 kwa mwaka ili kutunza mazingira.
Gambo alitoa hutuba hiyo kwenye maadhimisho ya upandaji miti
mkoa Arusha ambayo yalifanyika kijiji cha Selela wilaya ya Monduli.
Katika hutuba ya Gambo ambayo ilisimwa na Mkuu wa wilaya ya
Karatu,Theresia Mahongo alisema ili kufanikisha hilo,kila halmashauri inapaswa
kutenga fedha kila mwaka.
"Tengeni fedha kila mwaka kusaidia kupanda miti na
kuihifadhi" alisema
Mkuu huyo wa mkoa alizitaka halmashauri kushirikiana na wadau
mbali mbali ili kufanikisha hilo zikiwepo sekta binafsi.
Awali Meneja Masoko wa kampuni ya Mobisol,David Ngwale ambao
walikuwa sehemu ya wadhamini wa zoezi hilo,alisema suala la utunzwaji mazingira
ni la watanzania wote.
Alisema kampuni yao ambayo huzalisha umeme wa jua itaendelea
kusambaza huduma huyo hasa maeneo ya vijijini ili kuzuia uharibifu wa mazingira
katika kupata nishati ya umeme.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Monduli,Steven Ulaya alisema wilaya
hiyo kwa kushirikiana na wadau ikiwepo Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro
imejopanga kukabiliana na uharibifu wa mazingira.
"Tumekuwa na miradi ya kupanda miti,kuhimiza majiko sanifu
na tunashukuru wadau kama Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro kusaidia" alisema.
Meneja wa malisho ya wanyama katika mamlaka ya hifadhi ya
Ngorongoro, Hillal Mushi alisema Mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na
serikali misitu na kulinda vyanzo vya maji.
Alisema NCAA pia imekuwa na miradi ya kusambaza miti bure
vijijini ili kuhakikisha mazingira yanatunzwa kwa manufaa ya sasa na vizazi
vijavyo.
Wadau kutoka Mobisol wakifuatilia hotuba
DC wa Karatu Mahongo akitoa chetiu cha utambuzi
Baadhi ya wadau wakifuatilia
No comments:
Post a Comment