1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo (katikati) akimskiliza mwananchi Salma Hoza
(mbele),akitoa maoni yake kuhusu huduma inayotolewa na Wakala wa mabasi yaendayo
haraka (DART).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo (katikati) akifuatilia mwenendo wa mabasi yaendayo haraka (hayapo pichani) yanayofanya kazi katika vituo vya kushushia na kupakia abiria.
1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo (kulia) akitoa maelekezo kwa wataalam wa wakala
wa mabasi yaendayo haraka (DART) wakati wa ziara yake katika vituo vya Mabasi hayo
kulia ni Mtendaji Mkuu wa DART, Leonard Lwekatare.
NteghenjwaHosseah –
Tamisemi – Dar es Salaam.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jaffo ameagiza wafanyabiashara wote wanaofanya biashara katika vituo
vya mabasi yanaendayo haraka waondolewe na watafutiwe maeneo maalumu ya kufanyia
kazi zao na halmashauri husika.
Waziri Jaffo ameyasema hayo wakati waziara yake katika vituo
vya mabasi yaendayo haraka vya Morroco na Kivukoni na kukuta wafanyabiashara ndogo
ndogo wakiendelea na shughuli ambazo kwa kiasi kikubwa zina haribu na kuchafua miundombinu
ya mabasi yaendayo haraka.
“Vituo hivi ni maalumu kwa
ajili ya abiria kusafirishwa mpaka maeneo wanapokwenda na sio biashara na kwasababu
vituo hivi viko kwenye halmashauri ambazo nazisimamia Mimi naagiza wafanyabiashara
hawa waondolewe na watafutiwe maeneo yatakayofaa kwa ajili ya biashara zao lakini
sio ruksa kufanyia biashara hizo katika eneo hili maalumu kwa ajili ya mabasi yaendayo
haraka,” alisema Waziri Jaffo.
Katika ziara hiyo Waziri
Jaffo aliagiza uongozi wa DART kufanya mazungumzo ya haraka na Jeshi la Polisi,
Kikosi cha Usalama Barabarani kuangalia namna bora ya kuongoza mabasi hayo kwenye
maeneo ya makutano ya barabara hususani sehemu zenye Taa za kuongozea magari na
ikiwezekana taa za barabarani zifanye kazi yake.
“NimepokeamalalamikotokakwawananchiambaondiowatumiajiwamabasikuwahusimamamudamrefukwenyemaeneozilipoTaazabarabaranikwasababuAskarianayaongozayeyenasiotaahivyohusimamamudamrefukusubiriaAskariayaruhusunakupotezamaanayakuwamabasiyaendayoharaka”
alisemaJaffo.
Aidha Waziri Jaffo aliutaka
uongozi wa DART kuongeza Kadi za kusafirishia abiria kwasababu imekuwa ni hitaji
kubwa sana na la muda mrefu la watumiaji wa usafiri huo: Hakikisheni mnakamilisha
mchakato huo mapema ili wananchi wapate huduma hiyo wanayo ihitaji.
Pia aliwasisitiza uongozi
wa DART kuwa elekeza madereva wa mabasi yaendayo haraka kuhakikisha wanachukua abiria
katika vituo vyote nasio kuwaacha abiria katika baadhi ya vituo kwasababu ya wingi
wa abiria hayo na yale Mabasi ya Express kutoka Kivukoni –Kimara na Gerezani-Kimara
kuchukua abiria wa Kimara tu nasi wale wa kushuka kwenye vituo vya karibu.
TAMISEMI YA WANANCHI.
No comments:
Post a Comment