Monday, October 23, 2017

TUNATEKELEZA-MERERANI WAPATIWA FEDHA ZA UBORESHAJI WA KITUO CHA AFYA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu Genesta Mhagama akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo wakati wa uzinduzi wa namba maalum ya kuchangia Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti ukimwi.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Genesta Mhagama amemkabidhi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selamani Jaffo Sh milioni 200,000 kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha Afya Mererani ikiwa ni ahadi ya Rais Dk. John Magufuli aliyoitoa wakati waziara yake mkoani humo mwezi uliopita.


Ujenzi wa Kituo hicho ambao utaboresha huduma za mama na mtoto pia nimaalumu kwa ajili ya kusaidia zaidi katika kutoa huduma kwa watu walioathirika na virusi vya ukimwi katika wilaya ya Simanjiro.

Ikiwa ni miongoni mwa wilaya zilizoathirika zaidi na virus vya Ukimwi haswa katika eneo la Mererani imeonekana inahitaji msaada wa haraka ili kudhibiti au kupunguza kabisa tatizo hilo katika jamii ya eneo hilo.

FedhahizozimetokakatikamfukowaudhaminiwaudhibitiwaUkimwiambaoulizinduliwamwishonimwamwakajananakuanzakazirasmiyakukusanyafedhakutokakatikavyanzovyandanikusaidiakatikamapambanodhidiyaUkimwi.

Akipokea Hundi hiyo Waziri wa Tamisemi Selemani Jaffo kabla ya kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joel Bendera amesema umefika wakati ambapo jamii ya watanzania wanapaswa kuunga mkono jitihada hizo ili kupunguza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Wakati huo huo Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS). Imezindua rasmi namba maalum ya kuchangia Mfuko huo wa udhamini wa Kudhibiti Ukimwi.

Katika uzinduzi huo ambapo mgeni Rasmi alikua Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Genesta Mhagama alitaja namba ya uchangiaji wa mfuko huo kuwa 0684909090 na kwamba kila mwananchi ana himizwa kuchangia Fedha ili fedha itakayopatikana isaidie watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi.

Katika hatua nyingine Waziri Mhagama alimkabidhi hundi ya Sh milioni 660 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwa ajili ya kununua dawa aina ya Contrimaxozole za watu wanaoishi na VVU.

Fedha zote hizo zimetoka katika Mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi.


No comments:

Post a Comment