kuogelea.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo (aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla ya
kuangalia eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Kisasa la
Kuogelea katika shule ya Msingi Osterbay, Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo
Harrison Mwakyembe akizungumza katika hafla ya kuangalia eneo lililokuwa limetengwa
kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Kisasa la kuogelea katika shule ya Msingi Osterbay,
Dar es Salaam.
1. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo (katikati) akiwa na Waziri wa habari, Sanaa
na Michezo Harrison Mwakyembe(kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Happy(
kulia) na walimu wa shule ya Msingi Osterbay wakati wa hafla ya kuangalia eneo lililotengwa
kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la kisasa la kuogelea.
WAZIRI JAFFO: TAFUTENI
ENEO LA KUJENGA BWAWA LA KIMATAIFA LA KUOGELEA
Waziri wa Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinonondoni Ally Happy sambamba na uongozi wa Manispaa hiyo kutafuta eneo maalumu litakalofaa
kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la kuogelea lenye viwango vya kimataifa litakalotumika
kufundishia vijana wa Kitanzania jinsi ya kuogelela.
Jaffo ameyasema hayo wakati
wa hafla fupi ya kuangalia eneo la shule litakalofaa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa
la kuoegelea litakalo fadhiliwa na chama cha kuogelea Tanzania.
Akizungumza katika hafla
hiyo Waziri wa habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Harrison Mwakyembe alisema kwa
kipindi kirefu watanzania tumekuwa tukiungaunga kwenye mashindano mengi ya kimataifa
kitu ambacho kimesababisha ushindi wetu kuwa wakusuasua kila wakati lakini sasa
tunataka tuweke miundombinu katika mashule ambayo itatoa fursa ya watoto kujifunza
kuogelea kuanzia ngazi za chini.
“Tuna vipaji vingi sana
katika nchi yetu lakini haviendelezwi mfano katika hili la kuogelea kule kwetu Mbeya
watu wanaogelea kwenye mito na wanajua vizuri lakini ukiwaleta kwenye mabwawa ya
kimataifa wataishia kushindwa kwa sababu hawana mbinu za kitaalamu za kushiriki
kwenye mchezo huo” alisema Makyembe.
Akipokea maombi ya kujenga
bwawa la kuogelea katika shule ya Msingi Osterbay Waziri wa Tamisemi Selemani Jaffo amesema amepokea na kukubali
ombi la kujenga bwawa la kuogelea lakini eneo la shule ya Osterbay ni dogo halitakidhi
mahitaji na viwango vya bwawa la kimataifa la kuogelea hivyo uongozi wa Manispaa
utafute eneo linguine kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.
Aliongeza kuwa ana washukuru
wafadhili kutoka Chama cha kuogelea Tanzania kwa kuamua kutoa msaada wa ujenzi wa
bwawa la kuogelea ili kukuza vipaji kwa watanzania wengi ambao wamekosa fursa hiyo
kutokana na ukosefu wa mabwawa ya kuogelea (Swiming Pools) katika maeneo mengi.
Pia amewaomba wafadhili
hao kuendeleza kutoa msaada huo nje ya mikoa ya Dar es Salaam na kufika mpaka
Dodoma katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo ambapo pana eneo la kutosha kwa
ujenzi wa bwawa la kimataifa na uhitaji ni mkubwa kwa kuwa wanafunzi wanaosoma hapo
ni muhimu wakapatiwa burudani (entertainment) mbalimbali baada ya kutoka masomoni.
TAMISEMI YA WANANCHI
No comments:
Post a Comment