Washiriki wa Kongamano la la Kimataifa kuhusu Lishe maeneo kame nchini
Washiriki wa Kongamano la la Kimataifa kuhusu Lishe maeneo kame nchini
-ARUSHA
WATANZANIA hususani watoto na akina mama wajawazito wametakiwa
kutumia zaidi mchicha nafaka kama chakula kitakachowaongezea viini lishe muhimu
kwa afya ya miili yao.
Wito huo umetolewa mjini Arusha wakati wa Kongamano la
linalojadili Afya na na Lishe bora liliwakutanisha wataalamu wa masuala ya
lishe kutoka ndani na nje ya nchi wakiwamo wanajamii.
Kongamano hilo lililoanza Agosti 6 na kukamilika Agosti 9, Mwaka
huu linafanyika hapa ambapo wataalamu wanabadilishana uzoefu kuhusu masuala ya
afya na lishe bora limeandaliwa na Shirika la World Vision Tanzania (WVT),
wakishirikiana na Taasisi ya Amaranth ya Marekani na ECHO.
Akizungumza kwenye kongamano hilo Mkurugenzi wa Uendeshaji
Miradi ya Shirika la World Vision Tanzania, Dk. Yosh Kaslima alisema kupitia
shughuli wanazofanya kwenye mikoa 13 na wilaya 36 wamebaini kuwapo tatizo la
lishe bora kwa watoto na mama wajawazito.
“Wananchi hawajui wawalishe nini watoto na akina mama
wajawazito, kwa hiyo tunatarajia kupitia kongamano hili washiriki watatoa na
kupokea elimu mimea gani ina virutubisho vitakavyowawezesha kuboresha afya za
watoto wakiwa wadogo,” alisema Kaslima.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika Kongamano hilo Mkuu wa Mkoa
wa Arusha Mrisho Gambo alisema, ujumbe wa kongamano hilo unaohamasisha lishe ni
muhimu kwani umekuja kwa wakati sahihi.
“Hii inakwenda sambamba na Sera ya Taifa ya Chakula na Lishe ya
mwaka (2007) inayohamasisha uhusiano wa chakula na lishe katika sekta
mbalimbali na utokomezaji wa utapiamlo hasa kwa watoto na kina mama,”
“Kumuelimisha kila mwananchi, aelewe kuwa ana wajibika moja kwa
moja kutunza afya yake na ile ya familia yake. Kujenga ushirikiano kati ya
sekta ya umma, sekta binafsi, mashirika ya dini, asasi za kijamii na jamii katika
kutoa huduma za lishe na afya,” alisema Gmbo kupitia kwa Katibu Tawala Mkoa wa
Arusha Richard Kwitega.
No comments:
Post a Comment