Gobole lililotengenezwa na watuhumiwa wa ujangiri wilayani Uvinza
Watuhumiwa manne wa ujangili wamekamatwa na bunduki aina ya
gobole na zana mbalimbali za kutengeneza silaha hizo wilayani Uvinza mkoani
Kigoma.
Akizungumza na mwandishi habari Meneja wa Taasisi ya uhifadhi ya
Friedkin Conservation Fundi Uvinza, mkoani Kigoma, Audax Karurama alisema
kukamatwa watuhumiwa hao wa ujangili ni matokeo ya kazi ya intelijensia baina
ya askari Friedkin Conservation Fund ambao wanamiliki kitalu katika eneo hilo
na askari ya wanyamapori.
Karurama alisema, katika maeneo ya Uvinza Msebehi
kwa ushirikiano na askari wa Wanyamapori eneo la kifura walifanikiwa kukamata
mtuhumiwa wa ujangili jangili akiwa na silaha aina ya gobore na
Fundi wa kutengeneza magobore. .
Alimtaja mtuhumiwa Hugo ambaye tayari anashikoliwa na jeshi la
polisi ni Majaliwa Ramadhan(59) Mkazi wa kibaoni uvinza.
"Huyu mtuhumiwa tumemkuta pia na
Goroli 20 Baruti 1/4 kilo Mitego miwili ya waya na
nyuzi za katani" alisema
Alisema katika msako huo wamefanikiwa kumkamata
fundi wa magobole polisi ,Laurent Sungura(55) akiwa na mtambo wake maeneo
mlubanga -basanza.
Katika msako huo eneo la Uvinza walikamata watuhumiwa wawili
Wino Emily na Zakia sinzi wote wa kijiji cha mvinza wakiwa na
gobole.
"Tumewafuatilia sana kwa ujanja wao wakaenda kusalimisha
gobore kwa mwenyekiti wa kijiji chao. wakabaki na Smg. Kwa hiyo bado
Tunawafuatilia kwa karibu ili kukamata hiyo silaha yao" alisema.
No comments:
Post a Comment