Friday, July 27, 2018

FREEDOM HOUSE YAWAWEZESHA WANAHABARI WA MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU MBADALA WA UPASHANAJI NA UPATIKANAJI HABARI -ALTERNATIVE MEDIA

SHIRIKA la Kimataifa la Freedom House linaendesha mafunzo kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii 'bloggers' kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa ajili ya kuwajengea uwezo wa namna ya kuendesha vyombo hivyo vya habari mbadala katika upashaji na upatikanaji wa habari, (Alternative Media).

Mafunzo hayo ya siku mbili ‘Julai 26 – 27,2018’ kuhusu Vyombo vya habari mbadala ‘Alternative Media’ yaliyoratibiwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) yanafanyika katika ukumbi wa Flomi Hotel mkoani Morogoro.

Awali akifungua mafunzo hayo,Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Freedom House Clarence Kipobota amesema kupitia mafunzo hayo waendeshaji wa mitandao ya kijamii watajifunza mbinu mbalimbali kuhusu namna ya kuendesha mitandao yao.

“Tutajengeana uwezo na kujadili na kuunda jukwaa moja la waandishi ambao wanatumia Alternative Media”,alieleza.


Mwezeshaji wa semina hiyo Bw. Daniel Lema akitoa mada kwa waandishi wa habari katika semina inayofanyika katika hoteli ya Flomi mjini Morogoro.
Mwezeshaji John Kaoneka akitoa mada katika semina hiyo kuhusu mitandao ya kijamii.
 

          
Afisa Mafunzo , Utafiti na Machapisho UTPC Victor Maleko akiwa katika semina hiyo. 
Picha mbalimbali zikionyesha washiriki wa semina hiyo
 

Waandishi wa habari wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina hiyo.

No comments:

Post a Comment