Mmoja wa Wakurugenzi Kampuni ya Mwiba Holdings, Abdukadir
Mohammed akielezea mipango ya uwekezaji wa kampuni hiyo wilayani Meatu mbele ya
wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa Manyara waliopotembelea kampuni hiyo.
WANANCHI
wa Mkoa wa Simiyu, Arusha, Mara, Shinyanga na Mwanza wametakiwa kuchangamkia
fursa zinazotokana na uwekezaji unaofanywa na Kampuni ya Kitalii ya Mwiba
Holding Ltd katika Pori la Akiba Maswa.
Mpaka sasa Taasisi ya Friedkin Conservation Fund (FCF), inayoendesha
Kampuni za Mwiba Holding, Tanzania Game Trackers Safaris(TGTS) na Wingert
Safaris imewekeza zaidi ya Sh Bilioni 670 katika maeneo tofauti ya kitalii
nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Wakurugenzi wenzake Abdulkadir Mohamed
alisema mbali ya uwekezaji huo, wanatarajia pia kuongeza uwekezaji wa kiasi cha
Sh bilioni 227 katika kipindi cha mwaka huu
"Tunatarajia kuongeza uwekezaji ila tunachoomba mazingira
bora ya uwekezaji kuondolewe migogoro katika maeneo tuliyowekezaji. Lakini pia
suala zima la uvamizi wa mifugo na kama kutakuwa na upungufu wa jambo loloye ni
vyema tukaelezwa,"alisema Mohamed.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akiwa kwenye ziara na Wajumbe
wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya CCM mkoa
na wilaya ya Meatu alisema, uwekezaji uliofanywa na kampuni hiyo umekuwa na
faida zaidi kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
“Mwiba
Holding wamekeza eneo la Hifadhi ya Jamii ya wanyamapori(WMA) ya Makao na eneo
la Ranchi Kijiji cha Makao, wanatoa Sh milioni 610 kwa vijiji saba
vinavyozunguka hifadhi kila mwaka, wanachangia misaada na kutoa kutoa ajira,”
“Kampuni hiyo, pia inachangia shughuli za maendeleo na hivi
karibuni, imetoa saruji mifugo 3000, mabati 1000 na zaidi ya Sh milioni 115 kwa
ajili ya kuchangia mfuko wa elimu wa mkoa wa Simiyu,” alisema Mtaka.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji Taifa, Jackson Yuma
alitaka uongozi wa serikali kutokubali eneo la makao liharibiwe kwa kuruhusu
mifugo kuingia ndani ya hifadhi hiyo.
Yuma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa CCM mkoa
wa Simiyu, alitaka serikali kwa kushirikiana na wawekezaji kuhakikisha maeneo
yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi yanatunzwa kwa gharama zote kwa faida ya
sasa na vizazi vijavyo.
Aidha, Mkuu wa wilaya ya Meatu, Dk. Joseph Chilongani
alisema wilaya hiyo imeanza kunufaika na wawekezaji wa sekta ya utalii hivyo
aliomba migogoro isiyo ya lazima itatuliwa haraka.
No comments:
Post a Comment