Thursday, March 1, 2018

WABIBI NI NGUZO YA TAIFA LA TANZANIA

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira katikati akipokea maandamano ya Wabibi zaidi ya 200 waliotembea kutoka Hoteli ya Mount Meru hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kuwasilisha sauti zao kwa serikali. Wabibi hao kutoka ndani na nje ya nchi baadhi yao wamekuwa wakiishi na wajukuu wenye maambukizi ya HIV na hivyo kujikuta wakiwa na mzigo mkubwa wa malezi katika kipato kidogo.

Baadhi ya Wabibi wakiwa katika maandamo kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha mara baada ya kuhitimisha mafunzo yaliyokuwa yakifanyika katika Hoteli ya Mount Meru





 Washiriki wa maandamano wakiendelea kubadilishana mawazo 
 Washiriki wabibi kutoka nje ya nchi pia walikuwapo kuwaunga mkono wabibi wa nchini  
 Baadhi ya maofisa wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na wengine wakisubiria kuwasili kwa mgeni rasmi Anna Mghwira Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kupokea maandamano hayo ya amani
 Mmoja wa Waratibu wa Kongamano la Wabibi Tanzania Esuvati (kulia) akimsindikiza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira kupokea maandamano ya wabibi kushoto ni Mwandishi wa habari wa Channel Ten Aristides Dotto akijadiliana jambo na RC Mghwira

 Waandamani Wabibi wakiingia ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha tayari kwa kukamilisha Kongamano lao lililofanyika katika Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha 

Waandamani Wabibi wakiwa mbele ya ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha 
 Mmoja wa waratibu wa Kongamano la Wabibi Tanzania lililofanyika katika Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha kabla ya kuhitimishwa kwa maandano yaliyoishia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha 
 Waandamani wabibi wakiwa wamsimama na mabango yao wakimsiliza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira 

Mwakilishi wa wabibi katika Kongamano la Wabibi Tanzania lililofanyika Hoteli ya Mount Meru na kuhitimishwa kwa maandamano hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Edith Tarimo akiwasalimia wabibi 
 Mmoja ya waratibu Esuvat wa Kongamano la Wabibi Tanzania akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira aliyepokea maandamano ya wabibi waliotembelea kutoka Hoteli ya Mount Meru hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha 
 Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Arusha akizungumza na wabibi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira akizungumza na wabibi walioshiriki Kongamano la Wabibi Tanzania lililofanyika katika Hoteli ya Mount Meru na kisha kufuatiwa na maandamano hadi kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha ili kuwasilisha kilio chao kwa serikali.

No comments:

Post a Comment