Washiriki
wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati wa mafunzo ya ya siku tano kwa Wakuu
wa Wilaya na Wakurugenzi kutoka Mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara,Tanga,Kilimanjaro
na Arusha.
Nteghenjwa
Hosseah,
-OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewaagizi Wakuu
wa Wilaya na Wakurugenzi wote Nchini kuhakikisha wanadhibiti mianya ya upotevu
wa mapato ya ndani inayotokana na na
matumizi ya mifumo ya kielektroniki.
Waziri Jafo ameyasema
hayo wakati wa kufunga Mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa
Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Pwani, Lindi, Mtwara na Arusha yanayoratibiwa na
OR-TAMISEMI kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi na kufanyika kwa siku Tano
mjini Dodoma.
Waziri Jafo amesema
kuna baadhi ya Halmashauri ambazo mashine zake za Kielektroniki hazipeleki
Fedha kwenye Akaunti ya Serikali na badala yake Fedha za makusanyo zimeelekezwa
moja kwa moja kwenye akaunti za watu binafsi hili ni kosa kubwa sana Kisheria
na linatakiwa kudhibitiwa haraka iwezekanvyo.
“Natoa mfano wa
Halmashauri ya Kilindi ambayo mashine yake moja haiingizi Fedha kwenye Akaunti
ya Serikali na badala yake fedha hizo zinaenda kwa watu wengine kabisa
nakuagiza Mkurugenzi wa Kilindi kuwasilisha taarifa ya ununuzi wa mashine za
Kielektroniki, mgawanyo wa mashine hizo kwa wahusika, matumizi yake, mchangua
wa mapato yaliyopatikana kwenye halmashauri baada ya manunuzi ya mashine hizo na hatua ulizochukua baada ya kubaini
kuwa mashine moja inapeleka Fedha Nje ya Mfumo Alisema Jafo.
Hili liwe somo kwa
Halmashauri zote Nchini, kuhakikisha viongozi mnafuatilia mashine za
kieleketroniki kama zimeunganishwa kwenye Mfumo wa Serikali na hakuna hata
senti moja inayopotea katika mazingira ya kutatanisha na pia maeneo mengine
yote ambayo yanaweza kusababisha upotevu wa Fedha za Serikali.
Wakati huo huo Waziri
Jafo amewatakata viongozi hao kwenda kusimamia miradi ya maendeleo
inayotekelezwa katika maeneo yao kuanzia ukarabati wa Shule Kongwe za Sekondari, Ujenzi wa
miundombinu katika Vituo ya Afya, Mradi wa uboreshaji wa Miundombinu kama
Mpango Miji Mkakati(TSCP) pamoja na Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP)
Amesema nataka kuona
Viongozi wangu mnashindana katika usimamizi wa miradi wenye maeneo yenu kila
mmoja akifanya vizuri na miradi yote ikatekelezwa kwa ubora unaotakiwa tutakuwa
tumewasaidia sana watanzania katika kuwafikia huduma bora na hili ndio deni
letu kubwa kwa wananchi lazima tuache Alama ya Maendeleo.
“Ktika ujenzi wa
miundombinu ya Afya miwsho ni Tarehe 30 nataka mradi huu ukikamilika tulete
mapinduzi katika Sekta ya Afya Nchini na kwenye hili tutashidanisha Halmashauri
na itakayofanya vizuri Ofisi yangu itatoa zawadi pamoja na Cheti cha Utambuzi
wa usimamizi bora wa Mradi wa Ujenzi wa Vituo vya Afya.” Alisema Waziri Jafo.
Kwenye Miundombinu msimamie ipasavyo miradi yote ya miundombinu
nataka miradi hii ibadilishe Sura ya Nchi Yatu mpaka ikifika 2020 mtu
aliyeondoka Nchindi miaka mitano nyuma akirudi apotee Akute Miji yetu
imebadilika kwa kuwa na barabara nzuri, Taa za barabrani kila, mifereji ya
kusafirishia maji ya mvua, madampo ya kisasa pamoja na Stendi za kuvutia aliongeza
Jafo.
Akizungumzia mafunzo
waliyoyapata Viongozi hawa Jafo amesema nategemea kutakua na mabadiliko makubwa
baada ya mafunzo haya, mmejifunza mengi sasa muende mkatekeleze kwa Vitendo,
mkasimamie Nidhamu ya Kazi, mkajali mipaka yeu ya kazi na mkaboreshe mahusiano
kwa maslahi mapana ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Awali akitoa Taarifa ya
mafunzo haya Kaimu Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Bw. Kadari Singo amesema
mpaka sasa Taasisi ya Uongozi imekamilisha mtiririko wa kutoa mafunzo kwa Wakuu
wa Wilaya na Halmashauri zote Nchini na wanaishukuru OR-TAMISEMI kwa
ushirikiano walioutoa katika kufanikisha mafunzo yaliyotolewa kwa awamu nne kwa
viongozi wa kanda mbalimbali.
Amesema kiongozi
akipita katika mafunzo haya hawezi kuwa kama alivyokuja mwanzoni kutakua na mabadiliko ya Kitabia
ambayo yatachangia sana kuwabadilisha wananchi wataoenda kuongozwa na zaidi Viongozi hawa watakua na uwezo
mkubwa wa Kuwaza Kimkakati ambapo mipango yao itakuwa na Tija katika maisha ya
wananchi wanaowaongoza.
Akitoa Neno la Shukrani
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe.RoseMery Staki amesema mafunzo haya ni tofauti na
yale waliokuwa wanapewa viongozi huko nyuma haya ni bora zaidi kwa kuwa
yanagusa mtu binafsi, kisha wanagusa katika Ngazi ya Uongozi kisha kuwafundisha
kama watanzania hivyo elimu waliyoipata hapa itasaidia sana katika kutatua
changamoto za kila namna ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo katika shughuli zao
za kila siku.
No comments:
Post a Comment