Wananchi kutoka kaya masikini katika Kijiji cha Enduleni, Tarafa ya Ngorongoro wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakiwa kwenye foleni ya kupokea ruzuku ya kila mwezi inayotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kutoka kwa Wajumbe wa Kamati ya Watoa huduma ngazi ya jamii (CMC)
Mkazi wa Kijijini cha Enduleni, wilayani Ngorongoro akihesabu fedha (ruzuku) yake ya miezi miwili aliyokabidhiwa na Wajumbe wa Kamati ya Watoa huduma ngazi ya jamii (CMC) kutoka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Mjumbe wa Kamati Watoa Huduma ngazi ya jamii (CMC), akimuelekeza mwananchi namna kuweka dole gumba kwenye fomu baada ya kuchukua fedha za ruzuku ya miezi miwili kutoka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Afisa Mfuatiliaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha Anthony John akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Endulen wilayani humo wakati wa kutoa fedha (ruzuku) ya miezi miwili kwa kaya masikini
Wakazi wa Kijiji cha Enduleni wakiwa katika foleni tayari kwa kupokea fedha (ruzuku) ya miezi miwili kutoka kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Afisa Mfuatiliaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha Anthony John kulia akihakiki majina ya wakazi wa Kijiji cha Enduleni Tarafa ya Ngorongoro wakati wa utoaji wa ruzuku kwa kaya masini
Natoip Lekiposh (kulia), akiwa nje ya nyumba yake anayoishi sasa baada ya kuachana na mumewe kisha kurejea kwenye boma la wazazi wake kitongoji cha Adarpo Kijiji cha Enduleni Tarafa ya Ngorongoro kwa sasa mama huyo wa watoto wanne ameingia kwenye mpango wa ruzuku zinazotoklewa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF
Natoip Lekiposh (kulia) na mtoto wake wakiwa nje ya nyumba yake aanayotarajia kuhamia hivi karibuni aliyoijenga kwa kutumia fedha ruzuku anayopokea kila mwezi kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)
Afisa Mfuatiliaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha Anthony John kulia akichukua taarifa kutoka kwa Natoip Lekiposh anayepokea ruzuku kutoka TASAF
Hii ni kabati ya asili ya vyombo kwenye nyumba anayoishi kwa sasa Natoip Lekiposh
Eneo hili ndipo anapohifadhia kuni
Natoip Lekipos akiwa ndani ya nyumba yake ya asili
Afisa Mfuatiliaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha Anthony John akitoka kwenye nyumba ya asili ya kabila la Maasai anaiyoishi mmoja wa wanufaika wa ruzuku Natoip Lekipos
Afisa Mfuatiliaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha Anthony John akijadiliana jambo na mmoja wa wanufaika wa ruzuku Natoip Lekipos kuhusu umaliziaji wa nyumba yake mpya aliyoijenga kwa kutumia ruzuku ya TASAF
Mnufaika wa ruzuku inayotolewa na Mpango wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), katika Kijiji cha Enduleni wilayani Ngorongoro mkoani Arusha Kiserian Lembirika akiwa nje ya nyumba yake ya bati aliyoijenga kwa kutumia ruzuku ya kila mwezi, pamebeni yake ni wajukuu wanaomtegemea
Afisa Mfuatiliaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha Anthony John akitoa elimu ya uanzishwa wa vikundi vya kuweka na kukopa kwa wakazi wa Kijiji cha Ngoile wilayani humo kabla ya kuanza kutolewa kwa ruzuku.
No comments:
Post a Comment