Tuesday, January 23, 2018

TAMASHA LA OKOA NEW GENERATION LAUTIKISA MJI WA MONDULI

Mkurugenzi wa Asasi ya OKOA NEW GENERATION Neema Mgendi akizungumza wakati wa tamasha lililoandaliwa na asasi hiyo kwenye viwanja vya polisi mjini Monduli na kuwashirikisha vijana kutoka kwenye Mabaraza ya Vijana wa Kata tatu pamoja na makundi mengine ya vijana.kushoto kwake ni Katibu Tawala wa wilaya ya Monduli Robert Siyantemi kwenye kofia

 Mkurugenzi wa Asasi ya OKOA NEW GENERATION Neema Mgendi akiteta jambo na Katibu Tawala wa wilaya ya Monduli Robert Siyantemi wakati wa tamasha la vijana lililofanyika kwenye Viwanja vya Polisi mjini Monduli 
Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTI), kilichopo Monduli mjini wakitoa burudani ya nyimbo wakati wa tamasha la vijana 
Baadhi ya makundi ya vijana waliohudhuria tamasha hilo wakifuatilia michezo iliyokuwa ikiendelea uwanjani hapo
 Baadhi ya makundi ya vijana waliohudhuria tamasha hilo wakifuatilia michezo iliyokuwa ikiendelea uwanjani hapo

Wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTI), kilichopo Monduli mjini wakitoa burudani ya nyimbo wakati wa tamasha la vijana 
 Mwanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTI), kilichopo Monduli mjini akitoa burudani wakati wa tamasha la vijana 
 Baadhi ya makundi ya vijana waliohudhuria tamasha hilo wakifuatilia michezo iliyokuwa ikiendelea uwanjani hapo
Msanii wa vichekesho Katarina wa Karatu akitoa buruduani kwenye tamasha la vijana pamoja na msanii mwenzake Kobonge Mdudu 
Mgeni rasmi katika Tamasha hilo, Katibu Tawala wilaya ya Monduli Robert Siyantemi akikagua timu za mpira wa miguu zilizoshiriki kwenye tamasha hilo lililofanyika viwanja vya polisi mjini Monduli 
Vijana wakike wakicheza mpira wa Pete kwenye mashindano ya tamasha la vijana yaliyofanyika viwanja vya polisi mjini Monduli, tamasha hilo liliandaliwa na Asasi ya OKOA NEW GENERATION  
Katibu Tawala wilaya ya Monduli, Robert Siyantemi akimkabidhi zawadi Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Kata ya Lashaine muongozo wa ufugaji wa kuku wa kienyeji, kulia ni Mkurugenzi wa OKOA NEW GENERATION Neema Mgendi 
Katibu Tawala wilaya ya Monduli, Robert Siyantemi akimkabidhi zawadi ya mpira kiongozi wa timu ya wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii (CDTI)
 Katibu Tawala wilaya ya Monduli, Robert Siyantemi mwenye (kofia), pamoja na Mkurugenzi wa OKOA NEW GENERATION Neema Mgendi wakiwa na timu ya mpita wa Pete ya wanafunzi wa CDTI Monduli.

 Katibu Tawala wilaya ya Monduli, Robert Siyantemi akizungumza na wachezaji wa timu Nne zilizoshiriki mashindano kwenye tamasha la vijana waliopo kwenye Mabaraza ya Kata lililoandaliwa na Asasi ya OKOA NEW GENERATION 

No comments:

Post a Comment