Sunday, December 17, 2017

MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO AZINDUA ZOEZI LA UPIGAJI CHAPA NG'OMBE KIMKOA WILAYANI NGORONGORO

 Mwanamke wa Kimaaasai akisogeza mifugo yake tayari kwa kupigwa chapa wakati wa uzinduzi rasmi kwa mkoa wa Arusha uliofanyika Kijiji cha Erikepus, Kata ya Nainokanoka wilayani Ngorongoro na kufadhiliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) 

 Afisa Mifugo kutoka Mamlaka yaHifadhi ya Ngorongoro NCAA Genald Marandu akimpiga chapa ngo'mbe wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo kijijini Erikepus Kata ya Nainokanoka 
 Afisa mifugo Mwandamizi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kitengo cha Tiba ya wanyama wa majumbani Tegemea Mnzava akimpiga Chapa ng'ombe wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo kwa mkoa wa Arusha 
 Baadhi ya makundi ya ng'ombe wa wakazi wa Kijiji cha Erikepus yakiwa kwenye folone tayari kwa kupigwa Chapa ikiwa ni zoezi la kitaifa kwa afugaji wote nchini
 Wananchi wa Kijiji cha Erikepus wilayani Ngorongoro wakisubiria mifugo yao kupigwa Chapa wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi hilo mkoani Arusha
 Afisa Mifugo kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Genald Marandu akisalimiana na Afisa wa NCAA Nyange pamoja na maofisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha walipokutana kwenye uzinduzi wa zoezi la upigaji chapa ngo'mbe 

 Naibu Waziri wa Mifugo, Abdallah Ulega aliyenyosha mkono, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambao kushoto pamoja na Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka mwenye kofia wakiangalia namna ng'ombe walivyokuwa wakipangwa tayari kwa uzinduzi wa zoezi la upigaji Chama lililofanywa na Mkuu wa Mkoa.
 Naibu Waziri wa Mifugo, Abdallah Ulega akimpiga chama ng'ombe wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi hilo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha 
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akimpiga chapa ng'ombe ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa zoezi hilo lililofanyika wilayani Ngorongoro
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwaangalia ng'ombe aliokwisha kuwapiga chapa tayari wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo wilayani Ngorongoro 


 Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka akijiandaa kumpiga Chapa ng'ombe wakati wa uzinduzi rasmi uliofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo katika Kijiji cha Erikepus Kata ya Nainokanoka
 Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo akimpiga chapa ng'ombe 

 Mkuu wa wilaya ya Monduli akijiandaa kumpiga chapa ng'ombe 
 Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Tarafa ya Loliondo Edward Maura akimpiga chapa ng'ombe


 Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dk Maurus Msuha kulia akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akifuatiwa na Naibu Waziri wa Mifugo Abdallah Ulega 
 Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka mwenye kofia akibadilishana mawazo na Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo wakati wa zoezi la upigaji chapa ng'ombe 
 Naibu Waziri wa Mifugo Abdallal Ulega katikati akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakifuatilia kwa makini zoezi la upigaji Chapa ng'ombe
 Viongozi wakiendelea na majadiliano mara baada ya kuzindua rasmi zoezi la upigaji chapa ng'ombe 



 Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka akimtambulisha Mkuu wa wilaya ya Monduli aliyenyoosha mkono kusalimia wananchi wakati wa zoezi la upigaji chapa ng'ombe, pembeni yake ni Naibu Waziri wa Mifugo Abdallah Ulega
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo naye alikuwapo kuhakikisha zoezi hilo linakamilika kwa amani na usalama 
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro akisalimia wananchi wakati uzinduzi rasmi wa zoezi la upigaji chapa ng'ombe wilayani humo 
 Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Tarafa ya Ngorongoro Edward Maura akisalimia wananchi 
 Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dk Maurus Msuha akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa zoezi la upigaji Chapa mifugo 

 Naibu Waziri wa Mifugo Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa zoezi la upigaji chapa ng'ombe kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
 Baadhi ya wananchi wakifuatilia hotuba za viongozi wakati wa uzinduzi wa zoezi la upigaji chapa ng'ombe wilayani Ngorongoro mkoani Arusha 
 Naibu Waziri wa Mifugo Abdallah Ulega kulia akizungumza na wananchi 
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua zoezi la upigaji Chapa ng'ombe kwa mkoa huo zoezi lililofanyika katika Kijiji cha Erikepusi wilayani Ngorongoro
 Zoezi lilichukua muda mrefu na hivyo kuwalazimu baadhi ya wananchi kuwa na muda zaidi ya kupumzika ili kusubiria mifugo yao ipigwe chapa
 Kijana huyu akiendelea kuwadhibiti ng'ombe wakati alipokuwa akisubiria zamu yake tayari kwa kuwapiga chapa


 Naibu Mhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Asangye Bangu alikuwapo kushuhudia zoezi la upigaji chapa ng'ombe 

No comments:

Post a Comment