Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha TANELEC kinachotengeneza Transfoma Zahir Saleh akitoa taarifa ya uzalishaji wa kiwanda hicho kwa Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani aliyefanya ziara ya kukagua na kujionea uzalishaji wa Transfoma kwa ajili ya miradi ya kusambaza umeme inayotekelezwa na Serikali.
Ambapo katika ziara hiyo, Dk. Kalemani aliagiza Wakandarasi wote walioshinda Zabuni za kusambaza umeme vijijini (REA), kuhakikisha wananunua Transfoma kutoka kiwandani hapo ili kuvinjengea uwezo viwanda vya ndani pamoja na kuongeza mapato kwa Serikali.
Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha TANELEC kinachotengeneza Transfoma Zahir Saleh akisikiliza baadhi ya ushauri na mapendekezo yaliyokuwa yakitolewa na watendaji kutoka Wizara ya Nishati waliokuwa wameongozana na Waziri Dk. Medard Kalemani kutembelea kiwanda hicho kilichopo jijini Arusha
Baadhi ya maofisa kutoka Serikali ya Mkoa wa Arusha,Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na wafanyakazi wa Kiwanda cha TANELEC wanaotengeneza Transfoma wakimsikiliza Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho Zahir Saleh hayupo pichani alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utendaji kwa Waziri Dk. Medard Kalemani aliyetembelea kiwanda hicho ili kujionea uzalishaji
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani katikati akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kushoto), pamoja na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha TANELEC Zahir Saleh
Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani akisaini kitabu cha wageni tayari kwa ziara yake ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza Transfoma cha TANELEC kilichopo jijini Arusha
Fundi wa kuitengeneza baadhi ya vifaa vinavyofungwa kwenye Transfoma akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani, kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na kulia ni Meneja Mkuu wa Kiwanda cha TANELEC Zahir Saleh
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha TANELEC Zahir Saleh akimuonyesha Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani namna Transfoma zinavyozalishwa
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha TANELEC Zahir Saleh akiwa na Waziri wa Nishati D. Medard Kalema aliyefanya ziara kiwandani hapo ili kujionea uzalishaji wa Transfoma unavyokwenda
Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha TANELEC kinyweshea maji mti uliopandwa kiwandani hapo na Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalema wakati wa ziara yake
Transfoma zilizozalishwa katika Kiwanda cha TANELEC kilichopo jijini Arusha zikipakizwa kwenye gari tayari kupelekwa kwenye maeneo yenye miradi ya kusambaza umeme nchini
No comments:
Post a Comment