Mhandisi wa Maji kutoka World Vision Tanzania, Juma Maingu akitoa maelezo ya kisima cha maji kinachotumia nguvu ya umeme wa jua kwa ajili ya kusukuma maji kwenda kwenye mahitaji mengine ya wananchi katika eneo hilo
WAJUMBE wa Mkutano wa mwaka wa kujadili masuala ya huduma za upatikanaji wa Maji Safi na Salama na Mazingira katika Ukanda wa Afrika Mashariki kutoka World Vision, wakiangalia moja ya matenki ya kuhifadhia maji yaliyojengwa na World Vision Tanzania katika eneo la Mang'ola wilayani Karatu mkoani Arusha
Mhandisi wa Maji kutoka World Vision Tanzania, Juma Maingu akiwaonyesha baadhi ya washiriki wa Mkutano wa mwaka wa kujadili masuala ya huduma za upatikanaji wa Maji Safi na Salama na Mazingira katika Ukanda wa Afrika Mashariki namna mfereji wa kusafirisha maji kwenda kwenye mashamba tayari kwa umwagiliaji.
Moja ya mifereji ya kupitisha maji kwa ajili ya umwagiliaji katika mashamba ya vitunguu yaliyopo Mang'ola wilayani Karatu, mfereji huo umejengwa na World Vision Tanzania ili kuwawezesha wakulima hao kupata maji kwa utahisi zaidi kwa ajili ya shughuli za kilimo
Ziara ya wajumbe wa mkutano wa mwaka wa kujadili masuala ya huduma za upatikanaji wa Maji Safi na Salama na Mazingira katika Ukanda wa Afrika Mashariki kutoka World Vision ikiendelea katika eneo la Mang'ola wilayani Karatu mkoani Arusha
Kiongozi wa masuala ya Ushawishi, Ulinzi wa mtoto, Imani na Maendeleo World Vision Tanzania Mchungaji Joseph Mayala (kushoto), akitoa maelezo kwa wajumbe wa mkutano wa mwaka wa kujadili masuala ya huduma za upatikanaji wa Maji Safi na Salama na Mazingira katika Ukanda wa Afrika Mashariki kutoka World Vision waliotembelea eneo la Mang'ola wilayani Karatu kwa ajili ya kujionea shughuli zinazofanywa na WVT.
Wajumbe wa mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mashamba ya vitunguu yanayotumia maji ya mfereji uliojengwa na World Vision Tanzania
Baadhi ya miradi ya maji inayowezesha kuhudumia jamii wilayani Karatu mkoani Arusha ambapo wajumbe wa mkutano wa mwaka wa kujadili masuala ya huduma za upatikanaji wa Maji Safi na Salama na Mazingira katika Ukanda wa Afrika Mashariki kutoka World Vision walipita kujifunza na kujionea namna unavyofanya kazi
No comments:
Post a Comment