MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini(TANESCO),Dk. Lugano Wilson akiwa na timu ya wafanyakazi wa Shirika hilo kutoka Ofisi ya Uhusiano Makao Makuu, Kitengo cha udhibiti wa upotevu wa Mapato Makao Makuu na Mkoa wa Arusha na kitengo cha usalama na wenyeji TANESCO Arusha kwenye operesheni maalum ya kuwafichua wezi wa umeme wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Dk. Lugano Wilson akijionea uharibifu wa miundombinu na wizi wa umeme unaofanywa na wateja wasio waaminifu wakati wa Oparesheni inayoendelea wilayani Arumeru na maeneo mengine mkoani Arusha chini ya usimamizi wa timu maalumu kutoka Makao Makuu ya TANESCO Dar es Salaam
Afisa Mwandamizi kutoka TANESCO Makao Makuu Lenin Kiobya mwenye jacket akimuonyesha Mjumbe wa Bodi ya Shirika hilo Dk. Lugano Wilson (katikati), namna wateja walivyojiunganishia umeme na kuupitisha kwenye mashamba huko Halmashauri ya wilaya ya Meru mkoani Arusha
Majadilianio yakiendelea wakati wa Oparesheni ya kusaka wezi wa umeme na wanaoharibu miundombinu ya Shirika la Umeme Nchini TANESCO mkoani Arusha
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Dk. Lugano Wilson akiangalia namna waya za umeme zilivyopitishwa kwa njia za wizi katika mashamba huko Halmashauri ya wilaya ya Meru mkoani Arusha
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Dk. Lugano Wilson akionyesha moja ya nyaya za umeme zilizokuwa zimeunganishwa kwa njia ya wizi na kutumika kwenye makazi ya watu Halmashauri ya wilaya ya Meru, mkoani Arusha
Ukaguzi ukiendelea katika moja ya nyumba zilizokutwa zikiiba na kuharibu miundombinu ya Shirika la Umeme nchini TANESCO, Halmashauri ya wilaya ya Meru mkoani Arusha
Majadiliano ya kuendelea na Oparesheni ya kusaka wezi na wateja wanaoharibu miundombinu ya umeme ya TANESCO Halmashauri ya wilaya ya Meru mkoani Arusha
No comments:
Post a Comment