Wednesday, October 18, 2017

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba atembelea ujenzi wa nyumba mpya za askari Polisi wa Kituo Kikuu cha Mjini Arusha, ujenzi wa nyumba hizo mpya unafanyika baada ya zile za awali kuteketea kwa moto hivi karibuni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Charles Mkumbo akiwaonyesha kasi ya ujenzi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba kushoto na Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro walipotembelea ujenzi huo ili kujienea kasi 
Waziri wa Mambi ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akishiriki ujenzi wa nyumba mpya za askari polisi wa Kituo Kikuu cha Mjini Arusha baada ya nyumba za awali kuteteketea kwa moto hivi karibuni

 Waziri Mwigulu Nchemba akiendelea na ujenzi 

Waziri Mwigulu Nchemba akipima vipimo vya ukuta wa tofauti aliyoipandisha wakati wa ujenzi wa nyumba mpya za makazi ya askari polisi wa Kituo Kikuu cha Mijini Arusha ambapo nyumba za awali ziliteketea kwa moto.
Ukaguzi wa ujenzi wa nyumba za askari polisi ukiendelea wakati Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba alipozitembelea hivi karibuni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba akiangalia baadhi ya Nondo zinazotumika kujengea makazi mapya ya askari polisi wa Kituo Kikuu cha Mjini Arusha 
Waziri Mwigu Nchemba akizungumza na wanahabari mara baada ya kutembelea ujenzi wa nyumba hizo  

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba akisalimiana na mmoja wa Wakurugenzi wa Mgodi wa Tanzanite One Faisal Juma ambao kampuni hiyo inajenga nyumba 18 za makazi ya askari polisi baada ya nyumba za awali kuteketea kwa moto, katikati ni Mfanyabiashara wa mjini Arusha Hans Paul ambaye naye ameshirikiana na wadau wengine kwenye ujenzi huo  

Waziri Mwigulu Nchemba akimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzanite One Faisal Juma wakati alipotembelea ujenzi wa nyumba mpya za askari polisi wa kituo cha mjini Arusha 
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanzanite One Faisal Juma katikati akijadiliana jambo na mfanyabiashara wa mjini Arusha Hans Paul na Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro mwenye kofia wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba aliyetembelea kujionea ujenzi wa nyumba mpya baada ya zile za awali kuteketea kwa moto

No comments:

Post a Comment