-ARUSHA
OPARESHENI saka wezi wa umeme inayofanywa na timu ya TANESCO Makao Makuu, imebaini kuwapo baadhi ya wateja Kijiji cha King’ori, Halmashauri ya wilayani Meru wanaofanya udanganyifu wa Mita za Luku na hivyo kutumia umeme bila kulipia gharama zozote.
Maofisa
hao kwa pamoja wameendelea na zoezi la kuwabaini wateja hao ambapo hulazimika
kuwakatia umeme huo wa wizi kisha kuwataka wafike ofisi za TANESCO zilizo
karibu yao ili wafanyiwe hesabu za madeni yao yaliyotokana na wizi na
malimbikizo mengine.
Fundi wa TANESCO akikata umeme uliokuwa umeunganishwa kwa njia za wizi kutoka kwenye mashine ya kusaga kwenda kwenye moja ya nyumba za makazi kijijini King'ori madukaniAfisa kutoka TANESCO akionyesha namna wateja hao walivyokuwa wameunganisha umeme kutoka kwenye mashine kwenda kwenye makazi jirani na jengo la mashine hiyo.
Maofisa wa TANESCO kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam wakiangalia waya wa umeme uliokuwa umeunganishwa na kuchimbiwa chini kutoka kwenye mashine ya kusaga kwenda kwenye nyumba ya makazi
Fundi wa umeme kutoka TANESCO akifukua waya wa umeme uliokuwa umechimbiwa chini
Afisa wa TANESCO kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam akichukua kumbukumbu muhimu kutoka kwenye nyumba iliyokuwa ikiiba umeme kijijini King'ori madukani
Afisa wa TANESCO kutoka Makao Makuu, Dar es Salaam akichukua maelezo ya mteja mwenye nyumba iliyokuwa imeunganishwa kutoka kwenye mashine na nyaya zake kuchimbiwa chini
Mafundi na maofisa wa TANESCO wakimuonyesha mteja mwenye nyumba iliyokuw inapokea umeme wa wizi uliochimbiwa chini namna ambavyo nyaya zilivyokuwa zimekatika na kuwa hatari ambayo ingemsababishia hasara yeye na mali zake.
"Angalia jinsi nyaya zilizokuwa zinaleta umeme kwenye nyumba yako zilivyokuwa zimekatika hatua ambayo ingeweza kusababisha hatari zaidi kwa maisha yako"
Mhandisi Hussein Mbulu kutoka Makao Makuu ya TANESCO Dar es Salaam akimpa maelezo mteja aliyekuwa akiwa anaiibia shirika hilo umeme kijijini King'ori madukani wakati wa oparesheni ya kuwasaka wezi wa umeme
Mmiliki wa nyumba ya biashara na makazi katika eneo la King'ori madukani iliyokutwa ikiwa imeunganishiwa umeme wa wizi akiweka saini kwenye maelezo baada ya kuridhika
Mhandisi Hussein Mbulu kutoka Makao Makuu ya TANESCO Dar es Salaam, akiendelea kufungua Mita ya Luku iliyotolewa kwenye moja ya nguzo kijijini King'ori ambapo ilikuwa ikiwa imechezewa
Lazima tutagundua tu haiwezekani waendelee kuibia shirika
Njooni muone walivyounganisha
Afisa Usalama Mwandamizi kutoka TANESCO Makao Makuu Dar es Salaam mwenye koti Lenin Kiobya akimpa maelezo mteja ambaye nyumba yake ikutwa ikitumia umeme wa wizi, kupitia Mita ya Luku iliyokuwa imecheweza.
Fundi wa TANESCO akisokota waya wa umeme baada ya kuukata kutokana na wenyewe nyumba kudaiwa kuchezea baadhi ya miundombinu
Maofisa wa TANESCO na mafundi wakangalia moja ya nyumba za mteja wao katika eneo la Unga Limited mjini Arusha ambaye naye alikuwa amechezea miundombinu ili kutumia umeme wa bure
Mhandishi Hussein Mbulu kutoka TANESCO Makao Makuu Dar es Salaam akimuonyesha mteja wa shirika hilo aliyepo Unga Limited mjini Arusha namna Mita ya Luku ilivyokuwa imechezewa ili kuingiza umeme bila kulipia.
No comments:
Post a Comment