Mmiliki wa Shule ya Usa River Academy amelazimika kutoroka kusikojulikana baada ya timu ya maofisa wa TANESCO kufika shuleni kwake ili kufanya ukaguzi wa matumizi ya umeme, ambapo walibaini Mita za Luku 4 amezifanyia udanganyifu ili kutumia umeme bila kulipia
Maofisa wa TANESCO wakisimamia zoezi la kukata umeme kwenye Shule ya Usa River Academy iliyopo Usa River wilayani Arumeru mkoani Arusha
Fundi kutoka TANESCO akikata umeme kwenye Transfoma inayopeleka umeme shule ya Usa River Academy iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha baada ya kujiridhisha na udanganyifu wa wizi wa umeme aliokuwa anaufanya mmiliki wa shule hizo, ambaye pia alilazimika kutoroka kusikojulikana akiwakweka maofisa hao.
Bube Mwakyanjala kutoka Kitengo cha Udhibiti Mapato Makao Makuu ya TANESCO Dar es Salaam akionyesha moja ya Mita za Luku iliyochezewa katika Shule ya Usa River Academy iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha
Fundi wa TANESCO akiendelea kuchimba mtaro kufuata waya wa umeme uliokuwa umeunganishwa kwa wizi katika Shule ya Usa River Academy iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha
No comments:
Post a Comment