Tuesday, October 24, 2017

WAZIRI Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangala ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kutoa maelekezo muhimu

    MAELEKEZO YA WAZIRI Dk. Kigwangala:

Jukumu la msingi ni utekelezwaji wa Ilani ya chama tawala. Jitihada za makusudi ikiwa ni pamoja na ubunifu unahitajika katika kufikia kiwango cha watalii milioni 2 ifikapo mwaka 2020. 

Spidi ya utendaji kazi lazima iongezeke na kuwa yenye kasi kubwa zaidi. Bado utajiri wa vivutio vya utalii haujatumika ipasavyo kuvutia watalii wengi zaidi nchini.


Wananchi lazima washirikishwe katika uhifadhi wa rasilimali tulizonazo. Tuwe na mbinu za kisasa za kuzuia ujangili kabla haujatokea badala ya kupambana nao wakati mnyama ameshapoteza maisha. Tuwekeze zaidi katika eneo la intelijensia ili kupata taarifa za uhalifu mapema zaidi.

Tuwekeze katika kuongeza mapato ya utalii pamoja na kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato lwa kutumia mifumo ya kielektroniki.

WAZIRI DK. KIGWANGALA
Tuwekeze zaidi katika kutatua migogoro baina ya hifadhi na wananchi. Tuzidi kuimarisha uhifadhi ili hifadhi zetu ziweze kuwepo kwa muda mrefu ujao. Ubunifu una hitajika katika kuitangaza vema nchi yetu kiutalii. Shirika lipanue wigo wa vivutio vya utalii ili kuwafanya wageni kukaa muda mrefu sana nchini.

Wananchi wanapaswa kufaidika na uwepo wa sekta ya utalii nchini. Ukanda wa Kusini lazima ufunguke kuvutia watalii wengi zaidi. Kuimarisha mfumo wa Jeshi usu. Kurekebisha mfumo wa viwango vya wahudumu wa sekta ya utalii wawe na viwango bora na usajili ili waweze kutoa huduma stahiki kwa watalii wanaotembelea nchi yetu.

Uzalendo, uadilifu na uwajibikaji ni muhimu katima utekelezaji wa majukumu ya umma.
 Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangala alipofanya ziara Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo jijini Arusha
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangala akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, wakati alipotembelea Makao Makuu ya Shirika hilo yaliyopo jijini Arusha 
Baadhi ya wafanyakazi wa TANAPA wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangala alipokuwa akizungumza na wafanyakazi hao Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Arusha 
 Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangala akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo lenye makao makuu yake jijini Arusha 

Baadhi ya wafanyakazi wakimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangala alipokuwa akizungumza na wafanyakazi hao Makao Makuu ya Shirika hilo jijini Arusha

No comments:

Post a Comment