Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Halmashauri ya wilaya ya Meru, mkoani Arusha na Afisa Maendeleo ya Jamii Saumu
Kweka akicheza ngoma pamoja na akina wa eneo la Kikatiti wilayani humo wakati wa wiki ya elimu ya watu wazima.
Kweka katika maadhimisho hayo aliitaka jamii ambayo haikubahatika kupata elimu kupitia mfumo rasmi basi waweze kutumia fursa hiyo kwani katika maendeleo ya sayansi na teknolojia bila kujua kusoma na kuandika itakuwa ni kazi ngumu kujikomboa kimaisha.
Alisema elimu hiyo ya watu wazima katika Halmashauri ya wilaya ya Meru inaendelea kutekelezwa katika vikundi mbalimbali vya ujasiriamali na vikoba.
Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Halmashauri ya wilaya ya Meru, mkoani Arusha na Afisa Maendeleo ya Jamii Saumu Kweka aliyekuwa mgeni rasmi kwenye wiki ya Elimu ya watu wazima akitoa zawadi kwa mmoja ya watu wanaosoma elimu hiyo ya watu wazima katika eneo la Kikatiti Halmashauri ya wilaya ya Meru, mkoani Arusha
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chemchem iliyopo Kikatiti Halmashauri ya wilaya ya Meru wakiimba wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Elimu ya Watu wazima yaliyofanyika wilayani humo
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chemchem iliyopo Kikatiti Halmashauri ya wilaya ya Meru wakiimba wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Elimu ya Watu wazima yaliyofanyika wilayani humo
Mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya Elimu ya watu wazima katika Halmashauri ya wilaya ya Meru mkoani Arusha, ambaye ni Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Halmashauri ya wilaya ya Meru, mkoani Arusha na Afisa Maendeleo ya Jamii Saumu Kweka akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi Chemchem iliyopo Kikatiti wilayani humo wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu ya watu wazima.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chemchem iliyopo katika Halmashauri ya wilaya ya Meru, mkoani Arusha wakishiriki kucheza katika maadhimisho ya wiki ya elimu ya watu wazima iliyofanyika Kikatiti wilayani humo.
No comments:
Post a Comment