Fundi wa TANESCO akikata umeme katika moja ya mashine za kusaga Kikatiti wilayani Arumeru mkoani Arusha
-ARUSHA
Oparesheni ya kusaka wezi wa umeme mkoani Arusha imebaini
kuwapo kwa asilimia kubwa ya mashine za kusaga katika Kijiji cha Kikatiti
Halmashauri ya wilaya ya Meru zinatumia umeme wa wizi.
Mafundi kutoka TANESCO, wakifanya ukaguzi kwenye moja ya mashine walizozikuta zikiiba umeme wa shirika hilo na kuendelea kulisababishia hasara kila mwaka.
Zoezi la kukunya nyaya za umeme zilizokuwa zimeunganishwa kwa njia ya wizi likiendelea katika moja ya nyumba zilizopo Halmashauri ya wilayani Meru mkoani Arusha
Timu ya maofisa kutoka TANESCO wakiendelea na ukaguzi wa baadhi ya nyumba zinazoiba umeme katika eneo la Kikatiti wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Hayo yanaendelea kugunduliwa kwenye oparesheni maalumu na
endelevu inayofanywa kwa ushirikiano baina ya timu kutoka TANESCO Makao Makuu
inayojumuisha Ofisi ya uhusiano Makao Makuu, Kitengo cha Uthibiti mapato na
Kitengo cha Usalama Makao Makuu pamoja na Mkoa wa Arusha.
No comments:
Post a Comment