Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo
(mbele),akifungua kikao cha kupokea taarifa ya tathmini ya ugatuaji wa madaraka
na mapendekezo ya awali ya Mpango wa Maboresho wa Sekta ya Umma Awamu ya Tatu.
DODOMA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jaffo amesema kuwa Sera ya ugatuaji wa madaraka kwa
wananchi imefanikiwa kwa kiasi kidogo hivyo kunahitajika kuiboresha zaidi ili
dhana hiyo iweze kuleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika mamlaka ya
Serikaliza Mitaa.
Ameyasema hayo wakati wa
ufunguzi wa kikao cha kupokea
taarifa ya tathmini ya Ugatuaji
wa Madaraka na Mapendekezo ya awali ya mpango wa maboresho ya sekta ya umma
awamu ya tatu (PSRP III) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano Hazina Mjini Dodoma.
Waziri Jaffo amesema kuwa dhana
ya ugatuaji wa madaraka ilianza kutekelezwa tangu mwaka 1998 lakini kwa kipindi
kirefu dhana hii hajaeleweka vizuri kwa wahusika ndio maana hakuna mafanikio
yaliyotarajiwa kwa kutambua hilo tumeona ni vyema tukafanya tathmini jinsi ambavyo dhana hii inaweza
kuboreshwa na kuleta mabadiliko kwa wananchi.
Amesema kuwa katika kipindi
hiki cha Serikali ya awamu ya tano Agenda kubwa ni kufanya mabadiliko ndani ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, lakini mabadiliko haya yatapatikana kama watanzania
kwa ujumla wetu wataielewa dhana kamili ya Ugatuaji wa Madaraka na kusimamia
utekelezaji wake.
“Kuna viongozi wa ngazi
mbalimbali katika Serikali ambao bado uelewa wa dhana ya ugatuaji bado ni mdogo
kwani suala la ugatuaji si la mwananchi tu ila viongozi ndio tuliopewa dhamana ya
kuhakikisha kwamba madaraka yanagatuliwa kwa kadiri inavyotakiwa katika kila
ngazi ya jamii.
Amesema kuwa viongoozi mbalimbali
wamepewa dhamana katika Wizara mbalimbali lakini inawezekana asijue nini
anatakiwa kufanya katika sehemu yake ya kazi katika suala zima la ugatuaji wa
madaraka jambo hili lilikuwa likileta mgongano katika utendaji kazi .
Waziri Jaffo amewataka
viongozi wanaoshiriki kikao cha kufanya tathmini ya Ugatuaji wa madaraka na mapendekezo ya awali ya mpango wa maboresho wa sekta ya umma awamu
ya tatu (PSRP III) kujadili kwa kina na kubainisha matatizo yaliyopo katika
dhana ya ugatuaji wa madaraka ili mapendekezo watakayowalisha yaweze kuboresha
zaidi Sera hii kwa manufaa mapana ya watanzania.
Amesema kuwa kila kiongozi
anatakiwa kuhakikisha dhana ya ugatuaji wa madaraka kwa wananchi inashuka
katika ngazi ya Mkoa, Wilaya, Tarafa,Kata, mpaka ngazi ya mtaa ili kuleta
maendeleo katika jamii;
Ugatuzi ufanyike katika maeneo yote kuanzia madaraka ya
kimamlaka, Kisiasa, Rasilimali zifikishwe chini kwa wananchi, mabadiliko ya
kimahusiano pamoja Utawala unaoanzia kwa wananchi na ambao unazingatia mawazo
na mapendekezo ya wananchi hao.
Wakati huohuo Naibu Katibu
Mkuu- Elimu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tixon Zunda amesema kuwa lengo kuu la kufanya tathmini ya hali ya Ugatuaji wa madaraka nchini ni kutathmini halisi ya ugatuaji wa
madaraka ilivyotekelezwa kwa miaka
iliyopita na kupokea mapendekezo ambayo yatatumika kuandaa Sera mpya ya
Ugatuaji wa Madaraka Nchini.
Amesema kuwa utafiti huo
unatekelezwa kwa ufadhili wa shirika la
Maendeleo la Uingereza (DFID) ambapo Kampuni ya “The Law and Development Partnership L.TD”
imepewa jukumuikihusisha wataalam
washauri wa ndani na nje ya nchi.
Awali akitoa neno la
utangulizi Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof.Joseph Semboja alisema kikao
hiki ni muhimu kwa ustawi wa Taifa letu na kimejumuisha baadhi ya Wakuu wa
Mikoa, Wilaya, Wakurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na baadhi ya Wakuu wa Taasisi za umma na binafsi.
Kikao hiki cha kupokea Taarifa
ya ugatuaji wa madaraka na mapendekezo ya awali ya mpango wa maboresho wa Sekta
ya Umma awamu ya Tatu umeandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na
Taasisi ya Uongozi.
TAMISEMI
YA WANANCHI
No comments:
Post a Comment