Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli Stephen Ulaya akiwaonyesha namna juhudi za kuokoa bwawa kwa ajili ya matumizi ya mifugo na binadamu lililopo Kijiji cha Miserani Chini, timu ya wataalamu kutoka serikali (TASAF) waliotembelea kuangalia mafanikio ya Mpango wa kunusuru Kaya maskini.
Mifugo ikinywa maji kupitia mpango uliobuniwa na wananchi wa Kijiji cha Miserani Chini kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya maskini TASAF. Mradi huo umewasaidia wananchi kuhamisha maji kutoka kwenye Bwawa kwenda pembeni kulikowezesha mifugo kunywa maji bila kuchafua wala kuharibu bwawa.
Mkurugenzi wa Uratibu kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Issa Ibrahimu Mahamud ambaye ni Mjumbe wa timu ya Serikali (TASAF), iliyotembelea wananchi wa Kijiji cha Meserani Chini wilayani Monduli mkoani Arusha.
Mjumbe wa timu maalumu ya Serikali iliyoundwa kwa ajili ya kufanya tathimini na kukusanya maoni namna ya kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kitakavyokuwa.
No comments:
Post a Comment