Friday, September 29, 2017

WAKULIMA wa vitunguu Bonde la Ziwa Eyasi, wilayani Karatu mkoani Arusha wamelalamikia utaratibu wa ujazo 'Rumbesa', unaotumiwa na wakulima katika maeneo wa maeneo mengine kwani umekuwa ukiwasababishia hasara.

 Wakulima wa Vitunguu katika Bonde la Ziwa Eyasi,wakichambua vitunguu juzi wakati walipovuna baada ya kunufaika na mradi wa mjiundombinu ya maji katika Bonde la Ziwa Eyasi, wilayani Karatu mkoani Manyara

Meneja wa Mradi wa Dream Village kutoka Shirika la World Vision,Karatu, John Massenza akiwaelezea mradi wa maji Ofisa Mawasiliano Melickzedeck Karol wa World Vision Taifa na Nancy Okwengu Meneja Mawasiliano wa Shirika hilo,aAfrika Mashariki,namna mradi huo ulivyowasadia wakulima wa vitunguu katika Bonde la Ziwa Eyasi juzi.

WAKULIMA wa vitunguu Bonde la Ziwa Eyasi, wilayani Karatu mkoani Arusha wamelalamikia utaratibu wa ujazo 'Rumbesa', unaotumiwa na wakulima katika maeneo wa maeneo mengine kwani umekuwa ukiwasababishia hasara.


Wakulima hao waliyasema hayo juzi wakati wa ziara ya maafisa mawasiliano wa Shirika la Wolrd Vision kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini,waliotembelea vijiji vya Mbuganyekundu,Jobaj na Dumbechand,Kata ya Baray.

Aidha maafisa hao walitembelea vijiji hivyo vilivyopo Kata ya Baray ,ambavyo vinanufaika na mradi wa Dream Village,unaofadhiliwa na shirika hilo.

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wenzake Ramadhan Daudi,alisema kuwa serikali ilikataza ujazo huo wa rumbesa ila bado kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wafanyabiashara kutoka maeneo mengine kuendelea kuuza kwa ujazo huo.

"Tunaomba serikali iweke utaratibu maalum tupime kwa mizani au mlingano sawa kwani wengine wanauza kwa ujazo wa rumbesa,sisi tunapata hasara kwani vya kwetu havi nunuliwi sisi tunaweka ujazo unaotakiwa si rumbesa,"alisema na kuongeza
 Maaofisa Mawasiliano wa Shirika la World Vision,wakifurahia jambo na mkulima wa vitunguu katika Kata ya Baray Bonde la Ziwa Eyasi, wilayani Karatu mkoani Arusha wakati walipowatembelea wakulima hao walionufaika na mradi wa ujenzi wa miundombiunu ya maji uliofadhiliwa na Shirika hilo
 Katibu wa Kikundi cha Nyota Njema,Neema Mbise,akimkabidhi Meneja wa Mradi wa Dream Village kutoka Shirika la World Vision,Karatu, John Massenza,hotuba ya kikundi chao ambacho kimefadhiliwa na Shirika hilo kwa lengo la wazazi kuweza kupata mitaji na kuhudumia watoto wao
Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Wolrd Vision nchini, Melickzedeck Karol,akizungumza jambo na wanakikundi cha Nyota Njema wa Kata ya Baray wilayani Karatu Mkoa wa Arusha,juzi ambao wamenufaika na mradi wa Dream Village unaofadhiwa na Shirika hilo (PICHA ZOTE NA JANETH MUSHI)

"Hii ni changamoto kubwa kwetu sisi  soko,kwani World Vision wametuwezesha na tunapata maji kwa ajili ya kilimo,mazao yanakuwa mengi lakini hatuuzi kwa sababu ya changamoto hiyo,"

Naye Meneja usimamizi wa Babati ambayo inafanya kazi katika wilaya ya Karatu na Babati,alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa wakulima ya namna ya kutumia pembejeo pamoja na kulima kilimo cha kisasa na kuondokana na kilimo cha mazoea.

Kuhusu changamoto hiyo ya rumbesa,alisema kuwa wana mkakati wa kuwaunganisha wakulima na wanunuzi wakubwa ili kuondokana na tatizo hilo pamoja na tatizo la walanguzi ambapo wanawahamasisha kuungana kwenye vikundi ili waweze kuuza mazao yao kwa pamoja.

Naye Meneja wa mradi huo,John Massenza alisema kuwa mradi huo ulioanza mwaka 2014 unatarajiwa kukamilika mwaka 2019,ambapo watahudumia wananchi zaidi ya 18,000 ambapo kati yao zaidi ya asilimia 54 ni watoto.

Alisema kuwa mradi huo umejikita kusaidia kaya maskini,kukuza uelewa kwa vikundi vya wakulima na kuwapatia mitaji ili wazazi waweze kusaidia watoto wao na mradi wa maji.

Katika ziara hiyo maofisa hao walitembelea wakulima walionufaika na miradi mbalimbali ukiwemo wa maji,ambapo wamejengewa miundombinu inayowawezesha kumwagilia vitunguu na vikundi vya kuweka na kukopa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Karatu,Theresia Mahongo,alikiri tatizo hilo la rumbesa kuwa changamoto kwa wakulima hao ambapo aliwaomba viongozi wa maeneo mengine kusaidia kuzuia suala hilo ili wakulima wote wanufaike.

"Tuliwahamasisha wakulima wetu wakaacha kufunga kwa rumbesa ila wakifika sokoni kama Kilombero,Arusha mazao yao hayanunuliwi kwa sababu ya ujazo wanaoweka wao ambao ndiyo unatakiwa kuwekwa na wakulima wote,"alisema

Na JANETH MUSHI

No comments:

Post a Comment