Wednesday, September 27, 2017

TIMU YA WATAALAMU KUTOKA SERIKALI ILIYOTEULIWA KUANDAA MAPENDEKEZO YA MUUNDO WA KIPINDI CHA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI (PSSN) KUPITIA AWAMU YA TATU TASAF YAPIGA KAMBI MAKAZI YA WAHADZABE

Timu ya wataalamu mbalimbali kutoka serikalini, wakiwamo viongozi wa serikali kutoka wilaya ya Karatu wakimsikiliza mkazi wa Kijiji cha Endamanghan wilayani Karatu mkoani Arusha Maria Hando akielezea mafanikio aliyoyapata kupifia Mpango wa kunusuru Kaya maskini, uliomuwezesha kuinua hali ya maisha na kumuongezea kipato ambapo mama huyo amekuwa akilima mahindi na maharagwe kwa ajili ya kujiongezea kipato kilichomuwezesha kujenga nyumba ya bati. 

Makamu Mwenyekiti wa Timu ya wataalamu ya serikali (TASAF), kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Ined Muntari wa kwanza kulia akisikiliza maelezo ya mradi wa kupanda miti ya matunda unaofanywa na jamii ya Wahadzabe kijijini Endamaghan wilayani Karatu mkoani Arusha, kulia kwake ni Mkuu wa wilaya hiyo Theresia Mahongo.Wajumbe wa timu hiyo walitembelea makazi ya jamii hiyo ili kupata maoni juu ya awamu nyingine ya mradi huo

Mmoja wa vijana kutoka jamii ya Wahadzabe kijijini Endamaghan akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Karatu Theresia Mahongo, wakati timu ya wataalamu kutoka serikali ilipotembelea jamii hiyo ili kupata mawazo namna ya kuboresha awamu nyingine ya mradi wa TASAF. Katikati ni Mkurugenzi wa Huduma za jamii na utafiti wa TASAF Makao Makuu Amadeus Kamagenge akifuatilia maelezo kwa makini.
Ofisa wa TASAF kutoka Makao Makuu Dar es Salaam akinunua salaha ya Jadi  (upinde na mshale) wakati yeye na timu ya wataalamu wenzake walipoitembelea jamii hiyo kijijini Endamaghan wilayani Karatu mkoani Arusha.
 Mmoja wa wanaume wa jamii ya Wahadzabe akiwa amesimama huku amekanyanga fuvu la mnyama Nyati akisikiliza maelezo kutoka kwa timu ya wataalamu iliyoundwa na serikali kwa ajili ya kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini.
Jamii ya Kihadzabe ikicheza ngoma za jadi wakati wa mapokezi ya timu ya wataalamu kutoka serikali iliyoteuliwa kuandaa mapendekezo ya Muundo wa kipindi cha mpango wa kunusuru kata maskini
Sehemu ya makazi yanayotumiwa na jamii ya kihadzabe katika Kijiji cha Endamaghan Tarafa ya Eyasi wilayani Karatu mkoani Arusha jamii ambayo inaishi kwa kuwinda wanyama na kuokota matunda
 Mnufaika wa Mpango wa kuinua hali ya maisha na kuongeza kipato Maria Gwandu akimsikiliza Mkurugenzi wa Huduma na Utafiti wa TASAF kutoka Makao Makuu Amadeus Kamagenge wakati timu ya wataalamu iliyoundwa na serikali ilipomtembelea nyumbani kwake kijijini Endamaghani wilayani Karatu mkoani Arusha, mama huyo tayari amefanikiwa kuendesha mradi wa kufuga mbuzi pamoja na kulima mahindi na maharagwe yaliyomsaidia kujenga nyumba ya bati tofauti na aliyokuwa akiishi zamani. 
Mkurugenzi wa Huduma na Utafiti kutoka TASAF Makao Makuu Amadeus Kamagenge akijadiliana jambo na wakazi wa moja ya nyumba zilizopo kijijini Endamanghani zinazokaliwa na jamii ya Kihadzabe
 Sehemu ya shamba la maharagwe linalimilikiwa na mmoja wa wanufaika wa mpango wa kuinua hali ya maisha na kuongeza kipato Maria Gwandu
 Timu ya wataalamu kutoka serikali (TASAF), wakipokea maoni kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Endamaghan 
 Mjumbe wa timu ya wataalamu kutoka serikali (TASAF), Elias Shija kutoka Wizara ya Kilimo na Mifugo akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Endamaghani wakati wa kuchukua maoni ya wananchi hao kuhusu ujio wa awamu nyingine ya mpango wa kunusuru kaya maskini 
 Wananchi wakufuatilia maelezo kutoka kwa wataalamu wa TASAF waliofika Kijiji cha Endamaghan kuchukua maoni ya wananchi juu ya kuboresha awamu nyingine ya mpango huo 
 Majadiliano kati ya timu ya wataalamu na watendaji yakiendelea kijijini Endamaghan wilayani Karatu mkoani Arusha 


 Mwananchi wa Kijiji cha Endamaghan, Tarafa ya Eyasi wilayani Karatu mkoani Arusha akipokea sehemu ya mgao wake kutoka Mpango wa Kunusuru Kaya maskini unaotekelezwa na TASAF 

Baadhi ya wananchi wanaonufaika na Mpango wa kunusuru kaya masikini kijijini Endamaghan Tarafa ya Eyasi wilayani Karatu mkoani Arusha wakiwa wamepanga foleni kusubiria kupokea mgao wa fedha

No comments:

Post a Comment