Thursday, September 28, 2017

MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Awamu ya tatu kupitia Mradi wa kupunguza umaskini TPRP-OPEC III katika Kijiji cha Endashag'wet Karatu mkoani Arusha

KIJIJI cha Endashang'weti ni miongoni mwa vijiji 39 vya wilaya ya Karatu vinavyonufaika na Mpango wa kunusuru Kaya maskini unaotekelezwa kupitia TASAF Awamu ya tatu. Kijiji kipo umbali wa kilomita 28 kutoka Makao Makuu ya Halmashauri ya wilaya ya Karatu.

Kijiji hicho kina wakazi wapatao 2,538 kati yao wanawake ni 1,243 na wanaume ni 1295 waishio kwenye jumla ya kaya 527 kwa mujibu wa Senda ya Taifa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012. Mradi wa ukarabati wa barabara ya jamii Kijijini Endashag'weti uliibuliwa na walengwa waliopo kwenye mpango kwa kupitia mkutanmo wao. Jumla ya walengwa waliopo kijijini na ambao wameshiriki katika utekelezaji wa mradi ni 95 kati yao wanaume ni 15 na wanawake ni 80
 Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Endashang'weti Raymond Mwasha akisoma taarifa ya fuoi ya ukarabati wa barabara ya jamii yenye urefu wa Kilomita 1.8 na ujenzi wa vivuko katika kijiji cha Endashang'wet


 Diwani wa Kata ya Daa Benedicto Modaha katikatika akiwa na viongozi wenzake wakisikiliza maelezo kutoka kwa timu ya Timu ya Serikali iliyoteuliwa kuandaa mapendekezo ya muundo wa kipindi cha pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF)
Ofisa kutoka Ikulu Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Timu ya Serikali iliyoteuliwa kuandaa mapendekezo ya muundo wa kipindi cha pili cha Awamu ya Tatu ya Mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) akizungumza na wakati timu hiyo ilipotembelea kujionea mradi wa daraja
 Diwani wa Kata ya Daa Benedicto Modaha kitoa shukrani kwa timu hiyo kufika kwenye eneo lao 

No comments:

Post a Comment