Tanzania inakabiliwa na changamoto ya Kiwango cha ulaji
mdogo wa nyama kutokana na bei kuwa kubwa ambapo kwa kipindi cha mwaka
2012/13 hadi 2016/17 ulaji wa nyama umeendelea kuwa kilo 12 kwa mtu Kwa
mwaka.
Ambapo kiwango hicho kimeongezeka kidogo kwa mwaka 2015/16 na
kufikia kilo 15 kwa mtu Kwa mwaka, huku Kiwango hiki kikiwa ni kidogo Sana
ikilinganishwa na kiasi kinachoshauriwa na shirika la chakula na kilimo (FAO)
kwa kilo 50 kwa mtu Kwa mwaka.
Hayo yalisemwa jana kwenye maonyesho ya nanenane ,Afisa
usajili mifugo toka bodi ya nyama Tanzania, Ezekiel Maro wakati akizungumzia
hali halisi ya ulaji nyama hapa nchini.
Aidha alisema kuwa, changamoto hiyo inachangiwa na gharama za
mifugo kuwa juu zisizoendana na gharama za uzalishaji hivyo kupelekea watumiaji
kutumia mboga nyingine.
Maro alisema kuwa, changamoto nyingine inayochangia ulaji kuwa
chini ni kutokana na wananchi wengi kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya faida
za ulaji nyama.
"kwa kweli tunahitaji kuongeza kiwango cha uzalishaji wa
nyama na ili wananchi waweze kula nyama kwa wingi tunashauri wafanyabiashara wa
nyama kutumia mizani ya kidigitali ili kuwawezesha walaji kuwa wengi zaidi
kutokana na mtu kupimiwa nyama kulingana na hela aliyonayo. "alisema Maro.
Naye Afisa nyama kutoka bodi hiyo, Edgar Mamboi alisema kuwa,
katika kipindi cha mwaka 2012 /2013 hadi 2015/2016 kiwango cha uzalishaji wa
nyama nchini kimekuwa kikiongezeka kwa wastani wa asilimia 0.85 huku kwa
mwaka 2016/2017 kiwango kikiongeza kwa takriban tani 69 .
Mamboi alisema kuwa, kushuka kwa uzalishaji hususani nyama ya
mbuzi, kondoo, kuku na nguruwe kumetokana na uhaba wa vyakula vya mifugo.
Alisema kuwa, wanaendelea na kampeni ya kuhakikisha wananchi wanakula
nyama safi na salama huku wakiendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara wa nyama
kuweka magogo ya plastiki au mashine maalumu kwa ajili Aha kukatia nyama sehemu
salama zaidi.
Kwa upande wa baadhi ya Wateja wakizungumzia kuhusiana na swala
la wafanyabiashara wa nyama kukata kwenye magogo waliwaomba kupitishwa sheria
maalumu ya kuwabana ili waweze kukatia kwenye vifaa vinavyotakiwa kwa usalama
wa afya zao pia.
No comments:
Post a Comment