Friday, July 14, 2017

ZIARA YA WAZIRI JENISTA MHAGAMA KIWANDA CHA MACHINE TOOLS

WAZIRI wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Walemavu Jenista Mhagama akitembelea Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools kujionea maandalizi ya utekelezaji wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF uliotoa Sh. Bilioni 1.6 za ujenzi wa Kinu cha Tani 400 cha kuyeyushia vyuma na kuboresha miundombinu ya umeme kiwandani hapo ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kuitaka Mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini kushiriki katika ujenzi wa viwanda. 

Meneja wa Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Adriano Nyakule akitoa maelezo kwa Waziri Mhagama kuhusu mashine mbalimbali, pembeni ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira. 


 Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF Daud Msangi akisikiliza maelezo ya namna kiwanda hicho kinavyozalisha vipuri mbalimbali kwa ajili ya mashine, GEPF imetoa kiasi cha Sh Bilioni 1.6 kwa ajili ya ujenzi wa Tanuru la kuyeyushia vyuma
 Baadhi ya mitambo iliyomo ndani ya Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools

Mafundi wa kuchonga vipuri na kutengeneza mashine mbalimbali katika Kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio kushoto akiteta jambo na Meneja Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa GEPF Daud Msangi pamoja na maofisa wa Kampuni ya KeyMedia Solutions. 






   


1 comment: