TUHUMA za wizi wa ndoo mbili zinazodaiwa kuwa na madini ya Vito ya Tanzanite zimechukua sura mpya baada ya Mkuu wa Ulinzi wa Kampuni ya Tanzanite One Abubakari Lombe kudai si jambo rahisi.
Kauli hiyo alitoa juzi mjini hapa alipokuwa akitoa ufafanuzi wa habari zilizolipotiwa na vyombo vya habari kuhusu wizi wa madini katika mgodi unaomilikiwa na mwekezaji Kampuni ya Sky Associate na Serikali kupitia Shirika la Madini nchini (STAMICO).
Akizungumza mazingira ya kiulinzi na usalama mgodini hapo Lombe alisema, si jambo rahisi kutokea kitendo cha wizi mkubwa wa madini hayo kwenye mgodi wanaomiliki.
“Mgodini kwetu kuna ulinzi mkali haiwezekani kutoka na madini kirahisi tu kama ilivyoelezwa. Lakini kinafanyika kwa sasa ni vita ya kibiashara baina ya wafanyabiashara wa madini na wachimbaji,"alisema Lombe.
Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini Adam Juma akitoa taarifa ya Kamati ya Mofisa wa Madini iliyoundwa kuchunguza madai hayo kwenye mgodi wa Tanzanite One, alidai tuhuma hizo hazikuwa na ukweli.
“Baada ya ofisi kupata tuhuma za kuibiwa kwa madini ya Tanzanite June 21, Mwaka huu, tuliunda kamati ya watu sita iliyokwenda kuchunguza ikiongozwa na Afisa madini mkazi wa Mererani Elias Muterani.
“Kamati ile ilifanya kazi kwa kushirikiana na vyombo mbalimbali na ikabaini taarifa ambazo zimekuwa sikisambazwa si sahihi. Tulipeleka wataalam kuchunguza ikiwamo kupima uzito wa madini yote yaliorodheshwa na kutazama uzito wake hatukubaini wizi,"alisema Juma.
Naye Mtaalam wa miamba kutoka STAMICO, katika mgodi huo, Agrey Gonde alidai baada ya kupata taarifa ya wizi walifanya ukaguzi wa haraka kwenye eneo la hifadhi ya madini na kubaini hapakuwa na tukio la wizi.
“Kama serikali tupo makini kuungalia mgodi huu tofauti na watu wanavyofikiria,tumeimarisha udhibiti na ukaguzi karibia kila siku.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment