RUFAA ya Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema(
Chadema),akipinga
uamuzi mdogo uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,katika kesi
ya kuhamasisha watu kukusanyika na kufanya maandamano ya UKUTA
kinyume cha Sheria, kuanza kusikilizwa Agosti 16,Mwaka huu.
uamuzi mdogo uliotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,katika kesi
ya kuhamasisha watu kukusanyika na kufanya maandamano ya UKUTA
kinyume cha Sheria, kuanza kusikilizwa Agosti 16,Mwaka huu.
Mawakili wanaomuwakilisha Mbunge huyo,waliwasilisha kwa njia ya mdomo
taarifa ya kusudio la kukata Rufaa Mahakama Kuu kupinga uamuzi huo
uliotolewa Februari 8 mwaka huu, ambapo mawakili hao walitaka kesi
hiyo ikasikilizwe Mahakama ya Katiba (Mahakama Kuu),mbele ya jopo la
majaji watatu kutokana na kuwa na masuala ya kikatiba kwenye hati ya
mashitaka.
Jana mbele ya Jaji Dk. Modester Opiyo,Rufaa hiyo ilipangwa kuanza
kusikilizwa ila ilishindikana baada ya Wakili John Mallya anayemtetea
Lema,kuieleza mahakama hiyo kuwa hawajajipanga kwa ajili ya kusikiliza
kesi hiyo,walijua kesi imepangwa kwa ajili ya kutajwa.
Wakili Mallya aliiomba mahakama hiyo kuahirisha rufaa hiyo na
kuipangia tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikiliza ambapo
mawakili hao watawasilisha hoja zao za rufaa.
Jaji Dk.Opiyo alikubaliana na ombi hilo la Wakili huyo na kuahirisha
rufaa hiyo hadi Agosti 26 mwaka huu,saa 4;30 asubuhi itakaposikilizwa.
“Agosti 16 mwaka huu saa 4;30 asubuhi mjiandae kwa ajili ya
usikilizwaji wa rufaa siyo kutajwa,”Alisema Jaji huyo
Aidha Mawakili wa upande wa Jamhuri hawakuwepo mahakamani hapo jana
wakati rufaa hiyo ikiahirishwa.
Awali Februari 8, mwaka huu,Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ilitoa
uamuzi wa pingamizi zilizowasilishwa na Mawakili wa Lema,katika kesi
ya jinai namba 352/2016,mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo,Benard
Nganga,ambaye alitupilia mbali pingamizi hiyo na kusema kuwa mahakama
hiyo ina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.
Hakimu Nganga alisema kuwa baada ya kusikiliza hoja za pande zote
mbili,mahakama iliendelea kukagua hati hiyo ya mashitaka ambayo inadai
kuwa Lema anashitakiwa kwa kosa la kushawishi kutenda kosa kinyume na
kifungu cha 390 na cha 35 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jianai
ambapo anadaiwa kuhamasisha watu kufanya kusanyiko na maandamano
isivyo halali.
Alifafanua kuwa baada ya kupitia hati hiyo na kwa mujibu wa kifungu
cha 390 kinaelezea mtu akihusika na kushawishi kosa,hata kama halina
madhara huyo mtu ni mkosaji huku kifungu cha 35 kikielezea iwapo mtu
akiwa hatiani kwa kosa hilo adhabu yake ni kifungo cha miaka miwili au
faini au vyote viwili kwa pamoja.
Akizungumzia hoja ya kuwa shauri hilo kuwa na viashiria vya kikatiba
na mashahidi kushindwa kujibu maswali kwa upande wa utetezi watakuwa
wamenufaika na mashahidi kushindwa kujibu maswali.
"Ushahidi wa jamhuri kushindwa kutolewa hautakuwa na madhara kwa
mshitakiwa bali utamfaidisha na hoja ya shauri kuwa na masuala ya
kikatiba,hoja hiyo huwezi kuitambua kwa kuangalia vifungu
alivyoshitakiwa navyo mshitakiwa na kama ni hivyo hoja hiyo iletwe
wakati wa utetezi kama kesi itafika hatua ya utetezi,"alisema na
kuongeza
"Pingamizi zinatupiliwa mbali na mahakama hii haijaona haina uwezo wa
kusikiliza hivyo tutaendelea na kesi ya msingi,"
Baada ya uamuzi huo Wakili Sheck Mfinanga,alisema kuwa hawajaridhika
na uamuzi huo na kuomba kuwasilisha notisi hiyo ambayo ina nguvu sawa
na rufaa.
Wakili huyo alisema kwa mujibu wa kifungu namba 361(1),(a) cha Sheria
ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA),wanaomba kupewa mwenendo wa kesi
hiyo pamoja na uamuzi huo mdogo uliotolewa ili waweze kuandaa rufaa
hiyo na kuwasilisha Mahakama Kuu.
"Tunaupinga uamuzi huu ulioutoa na tunaomba kuwasilisha notisi ya
kukata rufaa ambayo ina nguvu sawa na rufaa na tunaomba shauri
lisiendelee kwanza mpaka Mahakama Kuu ikasikilize rufaa yetu dhidi ya
uamuzi huu,"alisema Mfinanga
Januari 18 mwaka huu Mawakili hao wanaomtetea Lema,waliiomba mahakama
hiyo kuhamisha shauri hilo Mahakama Kuu mbele ya Jopo la Majaji
watatu kutokana na kuwepo kwa masuala ya kikatiba kwenye hati ya
mashtaka.
Aidha walidai kuwa shauri hilo lina viashiria vya kikatiba
vinavyotaka kutolewa uamuzi na Mahakama ya Katiba ambayo ni Mahakama
Kuu mbele ya jopo la Majaji watatu,hivyo mahakama hiyo ya chini haina
uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.
Walitaja sababu nyingine ya kuomba kesi hiyo isisikilizwe na mahakama
hiyo ni kuwa mashahidi hawako kwenye nafasi ya kuweza mujibu maswali
yanayohusisha katiba.
Januari 18 kesi hiyo ilikwama kuanza kusikilizwa baada ya mawakili wa
utetezi kudai kuwa na hoja za kisheria,ambapo shahidi wa kwanza, Mkuu
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani hapa (RCO), SSP George
Katabazi,alikuwa aanze ushahidi wake.
Mwisho
No comments:
Post a Comment