SERENGETI-MARA
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Professa Jumanne Maghembe, amewapokea
mabilionea 26 waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakiwa wamefuatana na
wenzi wao (26) katika ziara yao ya siku 3 nchini Tanzania.
Wageni hao ambao wanatoka katika Club ya Mabilionea Young
Presidents Organisation (YPO) wanatoka mabara yote duniani.
Ziara hii ni ushahidi kuwa Tanzanina sasa hivi inaongoza kwa
vivutio vya utalii barani Afrika na duniani.
Katika ziara hiyo ya nchi nane (8) ambazo ni: Uingereza, Rwanda,
Tanzania, Maldeves, Nepal, Bhutan, Rajastan na nchi moja nyingine, wageni hao
wamemwaga sifa kem kem kwa vivutio vya Tanzania.
Katika hafla ya Chakula cha jioni alichowaandalia Wageni wake,
Prof. Maghembe aliwakaribisha nchini Tanzania na kuwaambia kuwa maajabu ya
Dunia yamebebwa na hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
"Hakuna eneo lolote katika uso wa Dunia lenye mkusanyiko wa
wanyama wanaokula majani (herbivorous) na wale wanaokula nyama (carnivorous)
kama ilivyo katika mbuga hiyo ya Serengeti.
Aidha, Prof. Maghembe aliwaeleza wageni wake kuwa uhifadhi ni
gharama kubwa inayobebwa na Tanzania kwa niaba ya Dunia.
Aliwaomba wageni hao wawe Mabalozi wa kuitangaza Tanzania kama
eneo pekee la amani lenye vivutio vyenye ubora wa pekee duniani. Alisema hatua hiyo italeta watalii wengi nakuiongezea Tanzania
mapato.
Aidha, aliwaomba warudi tena kuwekeza nchini ili washiriki kwenye
uchumi unaokuwa kwa wastani wa asilimia 7 kwa kipindi cha miaka 15 sasa.
Ends
No comments:
Post a Comment