Monday, July 17, 2017

DC CHONGOLO, RPC ARUSHA WAIMARISHA USALAMA WA NCHI

Mkuu wa wilaya ya Longido mkoani Arusha Daniel Chongolo akijadili jambo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC), Charles Mkumbo katika Kata ya Kamwanga iliyopo mpakani mwa wilaya hiyo na Rombo mkoani Kilimanjaro, mpakani mwa Tanzania na Kenya. 





Na MWANDISHI WETU

KAMATI ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Longido mkoani Arusha ikiongozana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (RPC) Charles Mkumbo imetembelea Kata ya Kamwanga iliyopo mpakani mwa Longido na wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.

Kata hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi za kiusalama ambazo zinatakiwa kutafutiwa ufumbuzi kutokana na kuwa pembezoni mwa wilaya kiasi cha umbali wa kilomita 130 kutoka Makao Makuu ya wilaya.

Akizungumzia ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Chongolo alisema, ziara hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa.

“Tumekubaliana kufungua kituo kikubwa cha Polisi katika eneo hilo. Tayari ujenzi wake unaendelea na kwamba upo katika hatua za mwisho kabisa.

“Mbili tumekubaliana kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha mapema iwezekanavyo tunapata gari kwa ajili ya kituo hicho na mwisho tumekubaliana kuongeza udhibiti wa mpaka, udhibiti wa biashara haramu ya dawa za kulevya, magendo na biashara haramu ya usafirishaji binadamu,” alisema Dc Chongolo.

No comments:

Post a Comment