WACHEZAJI, makocha na waamuzi wa soka
la wanawake kutoka nchi mbalimbali duniani wanapanda Mlima Kilimanjaro kwa
ajili ya kucheza mpira kileleni mwa mlima huo ikiwa ni sehemu ya kuenzi
mchezo wa mpira wa miguu.
Msafara huo ni kutoka nchi za Marekani, Dubai, Sweden, Ujerumani,
Uingereza, Palestine, Jordan na Afghanistan umelenga kuhamasicha mchezo huo
kuwa sawa kwa wanawake.
Akizungumza mjini hapa jana mmoja wa wachezaji aliyewahi
kuichezea timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars Mwaka 2006 , Rajvi Ladha ambaye
kwa sasa anachezea timu ya IFA Academy ya Dubai alisema wamekuja nchini kuweka
rekodi mpya ya kucheza mpira kileleni mwa mlima huo mrefu barani Afrika
“Soka la wanawake Tanzania liko chini
tofauti na wanaume, tutatumia ziara hii kuhamasisha ili nao upewe kipaumbele sehemu
zote lakini pia kuwahamasisha wanawake wenye vipaji wajitokeze na kujiunga na
timu" alisem Rajvi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya kukuza na kuinua
vipaji kwa vijana ya Future Stars Academy, Alfred Itaeli alisema ili kuleta
uwiano kwa soka la wanawake wamefika kuionyesha dunia kuwa sok la wanawanke
linawezekana.
"Soka la wanaume ndilo limekuwa likipata kipaumbele
tofauti na wanawake sasa hawa wenzetu wamekuja ku kuhamasisha wanawake wasiwe
nyuma kuonyesha uwezo wao wa soka.Tunashukuru kwa wachezaji wetu wawili wamepata
nafasi ya kwenda kupanda mlima ambao ni Regina Marcel na Upendo Leonard,"
alisema Itael.
Alisema walitarajia timu ya wanawake ya Twiga Stars
ingeweza kuja lakini ikashindikana kwani wangekuja wangepata nafasi ya
kubadilishana ujuzi kwani wageni hao ni wataalamu wa soka na wengi wao
wanacheza mpira katika timu za za Taifa.
Naye Ailsa Dixson Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Nature
Discovery walioratibu safari ya wachezaji hao alisema walifanya mawasiliano na
kushauriana ambapo waliona umuhimu wa kupanda mlima kwa kushirikisha wachezaji
kutoka mataifa mbalimbali ili kuweka usawa kwa wanawake katika michezo huo.
Katika michezo miwili iliyochezwa
katika Uwanja wa TGT nje Jiji la Arusha,timu hiyo ya Equal Playing Field
ilishinda mchezo wa kwanza dhidi ya Arusha kombaine kwa mabao 3-0 na mchezo wa
pili zilitoka suluhu ya kufungana bao 1-1.
Kwa upande wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF,kupitia
kwa Ofisa habari wake Alfred Lucas alisema kushindwa kufika kwa timu ya Twiga Stars
kucheza kulitokana na kushindwa kuelewana katika baadhi ya mambo.
No comments:
Post a Comment