Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) pamoja na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa pamoja wamesaini
makubaliano ya kuanzishwa kwa Chaneli maalum ya Utalii itakayohusika na
kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa soko la ndani na nje ya nchi.
Makubaliano hayo yametiwa saini na Mkurugenzi Mkuu wa
TANAPA Allan Kijazi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Devota Mdachi, Mkurugenzi
Mkuu wa TBC Dk. Ayub Rioba na Kaimu Mhifadhi wa NCAA Asangye Bangu.
No comments:
Post a Comment