TUME ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini
imekamata magunia 168 ya dawa za kulevya aina ya Bangi.
Aidha, mamlaka hiyo ilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 20
waliokuwa wamehifadhi magunia hayo katika Kitongoji cha Engendeko kilichopo
Kijiji cha Losinoni wilayani Arumeru mkoani hapa.
Akizungumza mjini hapa jana Kamishna wa Intelijensia wa Mamlaka
hiyo Fredrick Kibute alisema, shehena hiyo ilikamatwa alfajiri ya kumakia jana
kwa ushrikiano wa ofisi yake na askari wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kambi ya
Oljoro.
Alisema mafanikio hayo yametokana na kupokea taarifa kutoka kwa
raia wema ambapo walituma kikosi maalum kwa ajili ya kufanya uchunguzi kabla ya
kwenda kuvamia eneo husika.
“Tulipodhitibitisha taarifa za vyanzo vyetu tulipanga safu ya
kikosi kazi kwenda kukamata bangi hiyo na tumefanikiwa kukuta kile tulichokuwa
tumeambiwa na raia wema,” alisema Kibute na kuongeza:
“Tuliondoka Saa 8 usiku jana kuelekea kijiji husika tukiwa na
maalum kutoka ofisini kwangu,wanajeshi na polisi ilipofika Saa10:00 alfajiri
tulifanikiwa kufika na kuanza msako wa nyumba kwa nyumba,” alisema .
Akielezea kuhusu mazingira ya kijiji hicho na kilimo cha bangi
Kibute alisema, Kitongoji cha Engendeko ni moja ya maeneo yaliyotia for a
kwenye kilimo cha bangi.
Kibute aliwataka wananchi wilayani Arumeru kuacha mara moja
kilimo hicho cha bangi huku akisisitiza kuwa kwa sasa wanapatwa kusoma alama za
nyakati badala ya kufanya kilimo hicho kwa mazoea.
“Wananchi wanaolima bangi waache haraka ninawataka wasome alama
za nyakati. Ipo sheria namba tano ya Mwaka 2010 ambayo kwa sasa inasimamiwa
kikamilifu,” alisema Kibute.
Kwa upande wake Luteni Moses Gimonge kutoka Kikosi cha 833
Oljoro JKT alisema kazi hiyo haikuwa rahisi kutokana na kijiji hicho kuwa
kwenye Jiografia ya milima na mabonde makubwa.
“Tumeshrki zoezi hili baada ya kupokea Makao Makuu JKT nchini
kushiriki oparesheni ya kukamata bangi na tumetii maelekezo na tumefanikiwa
kikamilifu licha ya eneo hilo kuwa na changamoto,” alisema ya mabonde
makubwa na milima,” alisema Luteni Gimonge.
Wilaya ya Arumeru imekuwa moja ya maeneo nchini yanayolima bangi
kwa wingi ambapo wilayani humo zaidi ya Vijiji 22 wananchi wake wamekuwa
wakitegemea kilimo cha bangi kuendesha maisha yao.
No comments:
Post a Comment