Na JANETH MUSHI,
-ARUSHA
MAHAKAMA ya wilaya ya Arusha imeahirisha kesi inayomkabili mmiliki
wa Shule ya Lucky Vincent Innocent
Mushi, hadi Julai 5,Mwaka huu kutokana na upelelezi kutokukamilika.
Mtuhumiwa huyo pamoja na mwenzake ambaye ni Mwalimu Mkuu
Msaidizi Longino Nkana waliounguliwa kesi na 78 ya Mwaka huu wanatuhumiwa kwa
makosa ya usalama barabarani ikiwamo kusafirisha watoto bila kuwa na vibali
muhimu.
Mushi aliburuzwa kwa mara ya kwanza Mei 12,Mwaka huu
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,ambapo anakabiliwa na
mashitaka manne ya usalama barabarani.
Mbele ya Hakimu Desderi Kamugisha,Wakili wa Serikali Alice
Mtenga,aliiomba mahakama hiyo kuahirisha kesi hiyo na kuipangia tarehe nyingine
kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokukamilika.
Watuhumiwa hao walikuwa wakitetewa na Wakili Method Kimomogoro
ambapo Hakimu Kamugisha alikubaliana na wakili huyo na kuahirisha kesi hiyo
hadi Julai 7,Mwaka huu.
Awali wakisomewa mashitaka yao Mei 12,Mwaka huu, Wakili wa
Serikali Rose Sule alidai mtuhumiwa wa kwanza Mushi anakabiliwa na makosa manne
wakati Nkana akituhumiwa kwa kosa moja.
Wakili Sule alidai kwamba Mushi akiwa Mkurugenzi wa Shule ya
Lucky Vicent anatuhumiwa kuendesha gari la abiria bila ya kuwa na Leseni ya
usafirishaji.
Alidai kuwa Mei 6, Mwaka huu katika eneo la Kwamrombo wilayani
Arusha mtuhumiwa huyo alifanya shughuli ya usafirishaji wa abiria akiwa ana
mmiliki gari aina ya Mitsubish Rossa T. 871 BYS.
Aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa kosa la pili linamkabili
mtuhumiwa huyo ni la kuruhusu kuendeshwa kwa gari bila kuwa na Bima (Road
Licence), ambapo Mei 6, Mwaka huu aliruhusu gari hilo kuendeshwa huku akijua
halina Bima.
"Kosa la tatu ni kushindwa kuingia mkataba na mwajiri wake
ambapo Mei 6, Mwaka huu ukiwa mmiliki wa gari hilo ulishindwa kuingia
mkataba wa ajira na dereva wako Dismas Joseph Gasper ambaye kwa sasa ni
marehemu,” alidai Wakili Sule alipokuwa akisoma mashitaka na kuongeza:
"Mtuhumiwa unakabiliwa na kosa la Nne ambalo ni la kubeba
abiria waliozidi zaidi ya 13 ambapo Mei 6, Mwaka huu ukiwa Mkurugenzi, Afisa
Msafirishaji na mmiliki wa Lucky Vicent ulibeba na kusafirisha abiria zaidi ya
13, kinyume cha sheria,” alidai.
Wakili Sule akisoma mashitaka kwa mtuhumiwa wa pili alidai
mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa Nkana anadaiwa kukandaa safari iliyozidi abiria
13 huku akijua ni kinyume cha sheria.
Alidai kuwa Mei 6,Mwaka huu mtuhumiwa huyo akiwa na nafasi ya
Mwalimu Mkuu Msaidizi na mwandaaaji wa safari hiyo aliruhusu kupakia
abiria zaidi ya 13 kwenye gari liliosababisha vifo vya watu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment