Wednesday, May 31, 2017

UNCDF YAWAJENGEA UWEZO MANISPAA, MAJIJI NCHINI

Na MWANDISHI WETU
-ARUSHA

SHIRIKA la Maendeleo ya mitaji la umoja wa Mataifa (UNCDF) imewajengea uwezo Manispaa na Majiji matano nchini, ili waweze kupanua wigo wa uwekezaji  kwa ajili ya kuboresha maeneo yao na kukopesheka katika soko la hisa.


Akizungumza jana  Jijini hapa Mkuu wa shirika la Maendeleo ya Mitaji la Umoja wa mataifa (UNCDF), Peter  Malika alisema wameamua kuendesha warsha ya kimataifa ya siku mbili kwa kushirikiana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  ili Manispaa na Majiji hayo yanufaike na masoko ya mitaji Tanzania kwa kuwekeza katika soko la hisa kwa kuuza vipande na kuutoa hati za dhamana.

Alisema   ni vizurimajiji na manispaa wakabaini njia nzuri za kutafiti miradi ya maendeleo ya kiuchumi na utoaji huduma hatimaye waboreshe maisha ya wananchi wao na kukuza vipato vya majiji na halmashauri zao.

“Majiji tuliokutanisha ni Mwanza,Arusha,Mbeya,Tanga na Dar  es Salaam,pamoja na manipsaa tatu za Kinondoni,Temeke, Ilemela na Dodoma zenye uwezo wa kuanza kuwekeza katika soko la hisa kwa kuuza hati za
dhamana za manispaa,”alisema.

Alisema UNCDF ipo katika nchi 48 Duniani kazi yake kubwa inafungua rasilimali za umma na binafsi hasa ngazi za nyumbani ili kupunguza umaskini na kusaidia maendeleo ya kiuchumi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho gambo akifungua warsha hiyo kwa niaba ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa, George Simbachawene, aliipongeza UNCDF na Mamlaka za serikali  za mitaa kwa juhudi za kutafiti njia mbadala zinazoweza kutumiwa na mamlaka za serikali za mitaa kuongeza mapato kwa ajili ya uwekezaji miradi ya maendeleo ya uchumi.

Alisema kutokana na mahitaji mengi ya malamlaka za serikali za mitaa yasioendana na fedha kinahitajika  kuzisaidia mamlaka ya serikali za mitaa,majiji na manispaa kuwa na njia mbadala za kuongeza mapato yatakayowezesha kugharamia majiji yanayokua kwa kasi kubwa.

Gambo alisema anatumaini baada ya warsha hiyo wajumbe wataweza kutoka na mikakati ya kifedha itakayopima faida na hasara ya kutoa hati za dhamana za manispaa katika mazingira ya Tanzania kwa kuchambua mahitaji,vigezo na masharti  katika maandalizi ya uwekezaji.

Alisema  UNCDF itawezesha manispaa na majiji kukabiliana na changamoto za kifedha kwa kuimarisha huduma za msingi za ndani,kukuza maendeleo ya uchumi nma kuongeza uthabiti wa ndani na hali ya hewa na majanga ya
kiuchumi.

“Mbinu inatambua kuwa uchumi wa taifa umeongezeka kwa kasi zaidi kwa muda wa muongo mmojauliopita hata hivyo uwekezaji duni katika ngazi za chini bado ni kikwazo kikubwa katika mabadiliko ya miundombinu ndani
ya manispaa,”alisema.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia, alisema wamekutana majiji matano Tanzania Bara na masispaa tatu, wanaongelea mambo ya uwekezaji  na  majiji haya yanatakiwa kwenda jkisasa zaidi tofauti na zamani.

Wanajadili namna bora ya kuwekeza ili waweze kukopa na kuendesha miradi mikubwa kwa ajili ya  kuingia soko la hisa kama kampuni binafsi na umma.


Mwisho

No comments:

Post a Comment