Tuesday, May 30, 2017
MAMBO YAMSHINDA OLE MEDEYE UDP
*Ajivua uongozi
Na ELIYA MBONEA
-ARUSHA
KAIMU Katibu Mkuu wa Chama cha UDP, Goodluck Ole Medeye ametangaza
kuachia ngazi kwenye nafasi hiyo.
Kupitia barua yake yenye namba UDP/HQ/05/02 29 Mei, 2017 kwenda kwa
Mwenyekiti wa Taifa John Momose Cheyo, Medeye alisema amefikia uamuzi
huo ili kuyapa nafasi pana masuala yake binafsi nay a kifamilia.
“Napenda kukujulisha rasmi kwamba ili nipate muda wa kutosha kufanya
shughuli za ustawi na maendeleo ya familia na jamii inayonitegemea
nimeamua kwa hiari yangu kujiuzulu nafasi hiyo ya Katibu Mkuu kuanzia
tarehe ya barua hii,” alisema Medeye katika barua hiyo.
Medeye katika barua hiyo aliendelea kuelezwa kwamba uamuzi huo
aliuchukua baada ya kumpatia Cheyo taarifa isiyo rasmi walipokuwa
kwenye kikao cha mashauriano cha Kamati Kuu ofisini Mei 25, Mwaka huu
“Natumia fursa hii kukushukuru sana wewe na Kamati Kuu ya Chama kwa
kuniamini na kunipa dhamana ya kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha
United Democratic (The United Democratic Party – UDP) kuanzia tarehe
18 Juni 2016 hadi sasa,” alisema katika barua hiyo na kuongeza:
“Natumia fursa kukushukuru sana kwa uongozi wako na ushirikiano
ulionipa muda wote nilipokuwa Kaimu Katibu Mkuu wa UDP,” alisema.
Katika barua hiyo pia Medeye aliwasilisha taarifa hiyo ya kujiuzuri
nafasi hiyo Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Kuondoka Medeye aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi
Mwaka 2010 hadi 2015 akichaguliwa pia Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo na Makazi katika serikali ya awamu ya Nne.
Hata hivyo ilipofika mwaka 2015 kati wa vuguvugu la uchaguzi Mkuu
Mwanasiasa huyo alikihama chama hiyo na kukimbilia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambapo nako hakukaa sana kisha
alikimbia Chama cha UDP.
MWISHO/
Labels:
ARUSHA NEWS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment