
Na ELIYA MBONEA
-ARUSHA
MFANYABIASHARA wa duka la kuuza vocha, simu na line Firoz Khan ametiwa hatiani na mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa kuisababishia harasa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) ya sh Milioni 200,290,500
Mbali ya kutakiwa kulipa hasara hiyo mfanyabiashara alitiwa hatia katika makosa sita aliyoshitakiwa nayo na kutakiwa kulipa faini ya Sh Milioni 5 kwa kila kosa, kuanzia la kwanza hadi la tano au kwenda jela miaka miwili.
Kwa upande wake kosa la sita ambalo ni la uhujumu uchumi mtuhumiwa huyo aliamriwa kulipa faini ya Sh Milioni 2 au kwenda jela mwaka mmoja.
Akisoma hukumu hiyo jana mjini hapa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Arusha Desdery Kamugisha alisema ametoa adhabu hiyo baada ya kusikiliza pande zote mbili katika kesi hiyo.
Alisema mtuhumiwa huyo alidaiwa kuingiza, kuunganisha na kuendesha mitambo ya mawasiliano ya simu bila kuwa na kibali wala Leseni ya TCRA kosa ambalo alikiri mahakamani hapo
Awali mahakamani hapo kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo Wakili waSerikali Jehovaness Zakaria aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kazikwa mtuhumiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu na wafanyabiasharawengine.
Alidai mtuhumiwa huyo si tu aliathiri uchumi wa nchi bali piaalihatarisha usalama wa taifa kwa kuingilia mawasiliano ya simu bilakuwa na kibali wala leseni, hasa katika kipindi hiki cha mitandao namagenge ya ugaidi.
“Mheshimiwa Hakimu tunaiomba mahakama yako imchukulie hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine lakini pia mali na vifaa vyote vilivyoko hapa vitaifishwe na serikali,” alisema Wakili Zakaria.
Kwa upande wake Wakili wa utetezi Robert Rogatus aliiomba mahakama hiyo kutoa hukumu ya wastani kwa mteja wake kwani ni mtu anayetegemewa na jamii pamoja na familia.
“Mtuhumiwa ametoa ushirikiano katika shauri hili, hajasumbua mahakama pia ametoa ushirikiano kwa kukiri kosa na kurahisishia waendesha mashitaka kazi pamoja na kuomndoa gharama ambazo zingeigharimu serikali,” alidai Wakili Rogati na kuongeza:
Hata hivyo mara baada ya huku hiyo kutolewa Mwanasheria Mkuu Mwandamizi wa TCRA Johaness Karungura alisema upande wa Jamhuri umerishwa na hukumu hiyo na hautarajii kukata rufaa.
“Tunafurahia adhabu hii ni kubwa na itatoa fundisho kwa wale wote wanaohujumu mitandao ya simu. Niwaombe Watanzania kuelewa kwamba teknolojia haidanganyi kwani ukikamatwa hutakuwa na namna ya kukwepa,” alisema Mwanasheria Mkuu Karungura na kuongeza:
“TCRA inatumia fursa hii kuwatahadharisha watu wote wanaochezea mawasiliano kuacha mara moja kwani hatutakuwa na huruma kwa atakayechakachua mawasiliano au au kampuni ya simu itakayofanya udanganyifu kwenye laini za simu,” alisema.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment